Chuo Cha uhasibu Arusha (IAA)kimeshika nafasi ya pili kitengo cha elimu katika maonyesho ya nanenene kwa Kanda ya kaskazini Mkoani Arusha

Akizungumza Mara baada ya kupata kikombe hicho juzi Mkuu wa Chuo hicho Prof Eliamani Sedokeya amesema Siri ya ushi huo ni namna walivyojipanga katika banda lao kuelimisha vijana juu ya ujasiriamali utokanao na kilimo

Alisema kuwa katika banda la uhasibu waliweza kuwaweka pamoja vijana wanajihusisha na ujasiriamali ili waweze kuonyesha bidhaa zao

"Sisi kama taasisi ya Elimu na mafunzo tumekuwa tukitoa elimu kwa wajasiriamali hususani waliopo katika kilimo kwa kuwawezesha   kunoresha mazao yao ya biashara,kuwajengea uwezo wa masoko,utunzaji wa fedha na kumbukumbu"alisema Sedokeya

Pia alisema wamejipanga vizuri katika kuwawezesha vijana kuwa wajasiriamali na waone kilimo Kama  fursa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...