KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya ametilia shaka mienendo ya viongozi na watumishi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Karagwe na Kyerwa (KDCU) wakati wa Mkutano wake na viongozi wilayani Karagwe.

Akizungumza katika mkutano huo Kusaya amesema katika taarifa ya awali kutoka kwa wasamaria wema zimeonyesha kuwa kuna tuhuma za kuwepo kwa baadhi ya wanunuzi wa kahawa kutoa rushwa ili wauziwe kahawa kwa bei ya chini jambo linalochangia kudhulumu wakulima haki yao.

Kusaya amemtaja mmoja wa wanunuzi hao ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Mambo Coffee kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa jambo hilo linalodumaza maendeleo ya wakulima wa kahawa wilayani humo.

Kusaya amesema kwa nyakati tofauti viongozi na watumishi wa KDCU wamekua wakipokea fedha kwa njia ya simu na kwenye akaunti zao za Benki jambo linalodhaniwa kuwa ni kwa ajili ya kutekeleza nia ovu hiyo ya kushawishi kutoa upendeleo kwa wanunuzi binafsi.

Amemtaja Mhasibu Mkuu wa KDCU, Juvenary Burchard na Mtumishi mwingine Oscar Mjuni kuwa waliwekewa Sh Milioni 1 saa 2:07 usiku wa Machi 12 mwaka huu na Machi 14 wakaongezewa Sh Milioni Moja nyingine na Mtumishi mwingine, Whitney aliwekewa Sh Milioni 2.4.

Katika taarifa ya Katibu Mkuu pia ilionekana Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka nae aliwekewa kiasi cha Sh Milioni moja kutoka kwa mnunuzi wa kahawa wilayani humo na alipoulizwa lengo la kutumiwa fdha hizo hakusema zilitumwa kwa lengo gani.

Kusaya amewataka viongozi na watumishi hao wa KDCU kuwasilisha taarifa zao za Benki za kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu na kwamba zimfikie ofisini kwake Dodoma Agosti 30 mwaka huu.

" Kuna mashaka makubwa juu ya fedha hizi ambazo zinaonekana kuingizwa kwenye akaunti za wote niliowataja, maagizo yangu ni kwamba watumishi wote wa KDCU taarifa zenu za kibenki zinifikie kabla ya Agosti 30," Amesema Kusaya.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya akizungumza na viongozi na watumishi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Karagwe na Kyerwa (KDCU) alipofanya ziara ya kikazi wilayani Karagwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...