Bibi Rehema Hassan, mwenye Blauzi ya bluu kulia akiwaonyesha waandishi wa habari nakala ya hukumu ya Mahakam Kuu kitengo cha ardhi  iliyompa ushindi n kuamuru arudishiwe eneo lake lililopo eneo la Gogo Zingiziwa, Chanika jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni mtoto wake, Sophia Nassoro

KIKONGWE mwenye Umri wa miaka 80 mkazi wa Chanika Msumbiji, kata ya Zingiwa jijini Dar es Salaam, Rehema Hassan, amemuomba Rais John Magufuli amsaidie kupata eneo lake baada ya kushinda kesi mahakamani na kupewa tuzo kutoka Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi lakini wavamizi wamekaidi kutekeleza amri ya mahakama

MKAZI wa Chanika Msumbiji, Kata ya Zingiziwa, Rehema Hassan (80) amemuomba Rais Dkt.John Magufuli kumsaidia ili aweze kulikombea eneo lake lenye ukubwa wa 45 kwa 55 lililovamiwa na watu licha ya kushinda kesi mahakamani na kupewa tuzo kutoka Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi.

Akito kilio chake kwa waandishi wa habari,  Rehema amesema, amekuwa akimiliki eneo hilo lollipop Gogo kata hiyo ya Zingiziwa ambalo alinunua katika oparesheni ya vijiji tokea mwaka 1984 ambapo alilipata kwa kulima robo robo za operesheni vijiji na kisha kufanikiwa kununua eneo hilo.

Amesema, baadae alirithisha eneo hilo kwa watoto wake ambao mmoja alijenga nyumba yake lakini ikauzwa na mmoja alibomolewa nyumba yake, bila ya taarifa wakati yeye ndio mmiliki halali wa eneo hilo.

"Namuomba Rais Magufuli na Waziri wake aweze kunisaidia kwa hili kwa sababu wavamizi wanatumia nguvu ambayo mimi sina," amesema Rehema

Amesema, eneo lake, lilivamiwa na mtu anayeitwa kwa jina la Ramadhani Muguyumbi baada ya yeye kwenda kumuuguza mmewe kijijini Mengwa, Wilaya ya Kisarawe, Pwani, aliwakatia watu wengine na kuwuzia, baada ya kuona hivyo nilifungua kesi baraza la ardhi Ilala, na nikashinda kesi, " alisema. 

Amesema kuvamiwa kwa eneo lake limesababisha ajiulize mara kwa mara kuwa Mahakama ndogo zinaweza zikawa na nguvu za kuwarudisha watu waliyovamiwa eneo lake au Mahakama Kuu, kwa sababu haelewi wavamizi wanatoa wapi nguvu hiyo.

Mvamizi huyo (Muguyumbi) alikata rufaa Mahakama Kuu ya Ardhi mbele ya Jaji Haruna Songoro akipinga uamuzi wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Ilala  uliompa uhalali Rehema kwamba yeye ndio mmiliki halali wa hilo eneo. 

Hata hivyo, Rehema alishinda kesi hiyo. Katika uamuzi wake Jaji Songolo alisema amepitia kwa makini uamuzi ulitolewa baraza la ardhi na kumpa ushindi Rehema. 

Jaji Songolo alijiridhisha kuwa uamuzi huo ulikuwa sahihi na anaamuru kwamba, ardhi inayobishaniwa inamilikiwa na Rehema kama mabavyo Baraza la Adhi la Wilaya lilivyoamua na lirudishwe mikononi mwake haraka.

"Baada ya kupewa tuzo, tulirudishwa mahakama ya Ilala ambapo nilipewa dalali wa mahakama na alitekeleza amri ya kuwaondoa watu wote waliovamia eneo langu, lakini baada ya muda watu hao walimerudi tena upya," alisema 

Naye Sophia Nassoro mmoja ya watoto wa Rehem alisema mama yao ni mgonjwa, na ugonjwa wake unatokana na kupata mshtuko baada ya watu kuvamia eneo lake ambalo alilipata kwa jasho lake mwenyewe , jambo ambalo limesababisha kushindwa kumuhudumia.

"Mama yangu ni mzee sana na ni mgongwa tunaomba msaada wa Serikali kutumsaidi kupata eneo letu, kesi mahakamani tumeshinda, tuzo tumepewa lakini wavamizi wamerudi, tunaomba msaada wenyewe hatuwezi," alisema 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...