Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

KAMATI Ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imekifungia kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha Radio Clouds kuanzia leo Agasti 14 mwaka  huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Joseph Mapunda amesema, kufungia kipindi hicho ni kutokana na kukiuka maudhui ya Utangazaji mara kwa mara kupitia kipindi cha Jahazi licha ya kuonywa na kamati hiyo.

Mapunda amesema Radio Clouds walitangaza maudhui yasiyo  na lugha ya staha na yenye kuhamasisha vitendo vya ngono, kujichua na kupiga punyeto na kueleza kuwa kipindi hicho kilirushwa na kituo cha radio Clouds Juni 26, 2020 .

 Pia wametoa onyo kali na kuziweka chini ya uangalizi wa miezi mitatu kwa vituo vya Radio one Sterio na Radio Free Africa kwa kukiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha   matangazo ya Amka na  BBC kwa habari ya Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu ambaye aliituhumu Serikali kuwazuia viongozi wa chama hicho kutoshiriki kutoa heshima za mwisho za Rais Mstaafu Benjamin Mkapa huku kituo cha redio Abood FM kikiwekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita kwa kosa la kurusha mahojiano ya makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu bila kuzingatia mizani katika habari.

Vituo vilivyopigwa faini ni pamoja na Carry Mastory Media sh. Milioni tano,Triple  A FM sh.Milioni tano ,Wasafi Media Online Tv sh.Milioni tano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...