Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akipokea maelezo na kushuhudia hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa uwanja wa Majaliwa Stadium kutoka kwa viongozi wa Wilaya ya Ruangwa wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Hashim Mgadwila (aliyevaa suti) mnamo Agosti 12,2020 alipotembelea uwanja huo.

………………………………………………………………….

Na Shamimu Nyaki –WHUSM,Ruangwa

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison mwakyembe amei,pongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kwa ujenzi wa uwanja wa Majaliwa Stadium ambao unajengwa kwa kuzingatia viwango vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Dkt.Mwakyembe ametoa pongezi hizo Agosti 12,2020 alipotembelea uwanja huo ambapo amesema kuwa eneo la kuchezea (pitch) lina nyasi bora ambazo zina viwango vinavyohitajika katika viwanja vya soka duniani.

“Uwanja huu utakapokamilika utakuwa ni uwanja wa kisasa,kwasababu ujenzi wake unazingatia viwango vya kimataifa ikiwemo vyumba bora vya kubadilishia nguo, maduka ya kuuza jezi mbalimbali,majukwaa ya hadhi tofauti,hivyo Naipongeza sana Halmshauri ya Ruangwa kwa uwekezaji huu”alisema,Dkt.Mwakyembe.

Aidha Dkt.Mwakyembe ameishauri halmashauri hiyo kufikiria kuweka nyasi bandia katika uwanja huo kwakua nyasi hizo zinatumia gharama nafuu katika utunzaji na zinasaidia shughuli mbalimbali kufanyika bila kuharibika tofauti na nyasi halisi.

Vilevile Waziri Mwakyembe ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuilea vizuri timu ya Namungo FC ambayo imefanya vizuri katika ligi kuu na mashindano ya Kombe la shirikisho hatua iliyoifanya timu hiyo kufuzu kuiwakilisha nchi katika Kombe la shirikisho barani Afrika.

Kwa upande wake Afisa Mipango wa Halmshauri hiyo Bw.Fundikira Masamalo amesema kuwa uwanja huo utakua na majukwaa mbalimbali ikiwemo jukwaa kuu ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki takriban 1,200.

Uwanja huo unatarajiwa kuwa na viwango vinavyofanana na Uwanja wa Benjamin Mkapa wa Dar es Salaam na utatumika katika ligi mbalimbali na michezo mingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...