Na Said Mwishehe, Michuzi TV

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), kimesema wiki hii mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28,2020 atachuku fomu ya kuwania nafasi hiyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mjini Dodoma.

Akizungumza leo Agosti 5,2020 jijini Dar es Salaam , Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema mgombea wao wa nafasi ya urais atachukua fomu hiyo NEC wiki hii, na siku hiyo wataitangaza ili umma wa Watanzania uweze kufuatilia tukio hilo la kuchukua fomu kuomba ridhaa kwa mara pili.

"Napenda kuwatangazia rasmi kabisa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu John Magufuli ambaye sisi ndani ya Chama chetu na heshima kubwa ndio Mwenyekiti wa Chama chetu, lakini sisi kama Taifa la Tanzania tumepata bahati na tunashukuru Mungu sana, ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atachukua fumu wiki hii.

"Sasa ni lini ni vizuri nitawaambia tena maana na mimi napenda kuzungumza nanyi waandishi wa habari mara kwa mara kama sehemu ya kupeana taarifa, lakini wiki hii mgombea wa CCM, ndugu yetu, mpendwa wetu John Magufuli atachukua fomu kule jijini Dodoma.

"Na siku ya kuchukua fomu nitawatangazia ili macho yote yawe pale ndugu yetu akiomba dhamana kwa mara ya pili baada ya kuwa amefanya kazi nzuri sana iliyoyukuka, yenye kifani, iliyoandika historia na kuvunja rekodi sio tu Tanzania kwasababu kuna mahala tumechavuka viwango ulimwenguni kote,"amesema Polepole.

Amesisitiza kwamba Rais Magufuli anachukua fomu akiwa amefanya mambo makubwa na kuacha gumzo duniani ambapo ametolea mfano mapambano dhidi ya Corona ambapo Tanzania chini ya Rais Magufuli tumefanikiwa kushinda na kubwa zaidi Watanzania walijinyenyekeza kwa Mungu na kufanya maombi.

"Tumemtanguliza Mungu.Leo hii ndege kubwa kutoka Bara la Asia imetua nchini kwetu kwa ajili ya kuleta watalii, watalii wanaingia hapa na maisha yanaendelea.Kuna nchi leo hii bado ziko kwenye Lockdowwn.Corona ilikuwa ni janga kubwa, lakini Rais wetu alisema kwa Mungu ni dogo,"amesema Polepole.

Amefafanua zaidi sababu za kuibua kidedea kwenye vita ya
Corona kuna sababu tatu, moja ni kumtanguliza Mungu mbele."Tulisema sisi wa Tanzania na Rais wetu akiwa mbele kupambana na janga hili, tunakuachia wewe Mungu wetu wa mbinguni.Na sisi yale ya kibinadamu ikiwemo kuchapa kazi na kufuata ushauri wa kitaalam tutazingatia na Mungu wetu amejibu na leo hii tuko hapa tunaamani tele, tuaendelea kuchapa kazi.

"Kwa kweli kwa bahari ya Corona tumeishinda vita hii, Corona yenyewe ikikaa na wenzake wanatafakari kuhusu Tanzania. Ndio maana nisema leo , jana na juzi ndege kubwa kabisa kutoka ng'ambo na Asia zimeleta watalii,"amesema na kuongeza anatumia hiyo kueleza kwa niaba ya CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho na wasaidizi wake , kwa kweli wanamshukuru Mungu sana.

Ameongeza kwa hiyo mgombea wao atachukua fomu wiki hii, na ukweli atakwenda kufanya mambo makubwa zaidi katika muhula wake wa pili wa uongozi huku akifafanua mambo makubwa ya maendeleo ambayo yamefanywa na Rais Magufuli,hivyo watanzania watamchagua na ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuwa wa kishindo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...