Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Barnabas Samatta ameendelea na ziara yake ya kukagua maendeleo ya chuo hicho kwa kutembelea Kampasi ya Mbeya na kufurahishwa na maendeleo makubwa upande wa Taaluma na miundombinu.

Akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Prof. Matthew Luhanga, na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka; Mkuu huyo alipata fursa ya kupitia mpango wa matumizi ya Ardhi “Master Plan” ya eneo la Iwambi ikiwa ni sehemu ya mpango wa miaka 20 ya upanuzi wa Kampasi hiyo.

“Nimefurahi sana kuona mpango wa matumizi ya ardhi Iwambi kwa ajili ya upanuzi wa Kampasi ya Mbeya. Natamani sana kuona mpango huu ukitekelezwa na nipo tayari wakati wowote kutoa mchango wangu wa mawazo ili mpango huu uweze kutekelezwa kwa manufaa mapana ya wananchi wa Nyanda za Juu Kusini na Nchi jirani zinazotuzunguka” Alisisitiza

Ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya kuagana na wafanyakazi baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 11 tangu alipoteuliwa, amewapongeza Wafanyakazi na Wanafunzi kwa ushirikiano, na kwa kufanya kazi kwa bidii, kiasi cha kupelekea mafanikio makubwa katika kipindi kifupi, ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi na programu zinazofundishwa chuoni hapo, pamoja na upanuzi wa miundombinu ikiwemo kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Taaluma na  Utawala na jengo la  Maktaba.

Wakimwelezea kwa nyakati tofauti Wanafunzi na Wafanyakazi wa Kampasi ya Mbeya wamesifu na kupongeza umahiri wa Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta katika kusimamia maendeleo ya chuo hicho, na kwamba amekuwa chachu ya maendeleo ya haraka na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi kifupi cha uongozi wake.  

Mhe. Barnabas Samatta, yuko kwenye ziara ya kutembelea chuo hicho, kukagua maendeleo ya kitaaluma na ujenzi wa miuondombinu, ziara aliyoianza 23 Julai 2020, Kampasi Kuu Morogoro na atahitimisha Kampasi ya Dar-es-salaam kwa kukagua upanuzi wa miundombinu, shughuli za kitaaluma pamoja na kuzungumza na Wanafunzi na Wafanyakazi.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Barnabas Samatta akisalimiana kwa staili yake na mmoja wa viongozi wa Serikali ya wanafunzi (MUSO -Mbeya ) mara alipowasili chuoni hapo kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Chuo akiwa amekalia moja ya viti yanavyotumiwa na wanafunzi katika jengo jipya la Taaluma na Utawala, lililokamilika na kuanza kutumika. Wakishuhudia tukio hilo ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho na Mkuu wa Kampasi ya Mbeya Prof. George Shumbusho. 
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe akiwa ameambatana na Mkuu wa Kampasi ya Mbeya Prof. George Shumbusho na Menejimenti ya Chuo hicho wakati wa kukagua jengo jipya la Taaluma na Utawala lililokamilika hivi karibuni. 
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe akiwa ameambatana na Mkuu wa Kampasi ya Mbeya Prof. George Shumbusho na Menejimenti ya Chuo hicho wakati wa kukagua jengo jipya la Taaluma na Utawala lililokamilika hivi karibuni.
Wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya jengo jipya ni Menejimenti, Wafanyakazi wa Kampasi ya Mbeya na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta, baada ya kukamikisha ziara yake chuoni hapo.Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Barnabas Samatta akisalimiana kwa staili yake na mmoja wa viongozi wa Serikali ya wanafunzi (MUSO -Mbeya ) mara alipowasili chuoni hapo kwa ziara ya kikazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...