Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
AWAMU ya kwanza ya Ujenzi wa Mradi wa maji wa Jeti-Buza inaendelea kwa kasi ambapo mtandao wa bomba kwa umbali wa Kilomita 7.5 umeshatandazwa.

Mradi huo unaojengwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia fedha za ndani za Mamlaka na utahudumia wakazi wa maeneo ya Kiwalani, Vituka, Buza ,Machine namba 5 -Tandika na Mwanagati.

Wakiwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya mradi huo, Msimamizi  wa mradi huo Mhandisi John Romanus wa Dawasa amesema hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 85 hadi kukamilika kwake.

"Kazi ya ulazaji bomba imekamilika kwa asilimia 100 ambapo bomba la inch 16 limeshalazwa kwa umbali wa kilomita 7 kuanzia eneo la Jet corner mpaka njia panda ya Buza" alisema mhandisi Romanus. 

Aliongeza kuwa kazi zilizobaki ni uwekaji wa mfumo wa  kusafisha bomba (washout) pamoja kujengea mfumo wa kutoa hewa kwenye bomba (airvalve).

"Kazi hizi zinategemea kumalizika ndani ya miezi miwili kuanzia sasa hivyo kufanya mradi huu kufikia hatua za mwisho za utekelezaji wake "alimalizia mhadisi Romanus

Kwa upande wake Meneja mawasiliano Dawasa , Everlasting Lyaro alitoa wito kwa wananchi wa maeneo yatakayohudumiwa na mradi kupata taarifa sahihi kwa watendaji wa Kata na mitaa yao  ili kupata uelewa wa pamoja wa mradi na kuepuka taarifa zisizo sahihi. 

"Tunajua shauku kubwa ya wananchi wa huku wanaosubiri kuhudumiwa na Dawasa pindi mradi utakapokamilika. Nitoe rai kwa wananchi kutembelea ofisi za watendaji wa kata na mitaa yao ili kupata taarifa sahihi za mradi , utaratibu wa kupata huduma pindi mradi utakapokamilika na taarifa nyingine muhimu za Dawasa .

Akielezea kuhusu chimbuko la Mradi huo ni baada ya kukamilika kwa upanuzi wa Mtambo wa Ruvu Juu uliopelekea ongezeko la Maji

Amesema, Dawasa walianza ujenzi wa mradi huo baada ya Upanuzi wa mtambo wa Ruvu juu uliopelekea kuongeza kwa kiwango cha uzalishaji maji kutoka mita za ujazo 90,000 hadi kufikia mita za ujazo 180,000 .

Lyaro amesema, kutokana na ongezeko hilo, Dawasa wakaamua kuanzisha mradi mkubwa wa mtandao wa  maji kwa maeneo ya Dar es Salaam ya kusini.

"Lengo la mradi wa maji Jet-Lumo ni  kuhudumia wakazi wa maeneo ya Kiwalani, Vituka, Buza, mashine  namba 5-Tandika na Mwanagati ila kwa sasa tumeanza na awamu ya kwanza, ambayo inaenda kukamilika"amesema Lyaro.

"Mwaka wa fedha 2019/20 Dawasa kupitia mapato yake ya ndani ilitenga kiasi cha Bilioni 2.2 kwa ajili ya mradi huu ambapo kukamilika kwake  utahudumia wakazi takribani 173,810 wa kata za Yombo Vituka hadi Buza" alisema Lyaro

Nae mtendaji wa mtaa wa Magogoni kata ya Yombo Vituka, Bi Upendo Sinawi ameishukuru Dawasa kwa kuwalatea mradi mkubwa wa maji utakaoenda kuondoa adha ya kutumia maji ya visima ambavyo vingi havikuwa salama kwa wananchi. 

"Kwa miaka mingi eneo hili huduma ya Majisafi tunaipata kupitia visima vya watu binafsi au jumuiya ambavyo maji yake yanaweza kuwa na chumvi nyingi au yasiwe salama kwa matumizi ya binadamu.  Hivyo mradi huu wa maji ni mkombozi mkubwa kwa sisi viongozi wa wananchi kwani wananchi wetu watapata maji safi na salama kutoka Dawasa" alisema mtendaji huyo

Baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi, uendelezaji wa mradi kwa awamu ya pili utakuwa katika maeneo ya mashine namba 5-Tandika, Mwanagati,Kiwalani na baadae hadi Gongo la Mboto Jijini Dar es salaam.
 Msimamizi wa Mradi wa Jeti-Lumo Mhandisi John Romanus akitoa maelezo kaa Meneja wa Mawasiliano Dawasa Everlasting Lyaro wakati wa kutembelea mradi wa maji wa Jeti-Buza. 
 Msimamizi wa Mradi wa Jeti-Lumo Mhandisi John Romanus akitoa maelezo kwa Meneja wa Mawasiliano Dawasa Everlasting Lyaro (kulia) na Mtendaji wa mtaa wa Magogoni Upendo Sinawi wakati wa kutembelea mradi wa maji wa Jeti-Buza.


Mafundi wa Dawasa wakiendelea na kazi ya kulaza mabomba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...