Na Jusline Marco, Arusha
NAIBU waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhe.Atashasta Nditiye amewataka viongozi wa wilaya nchi ambazo reli inapita katika maeneo yao kufanya vikao na watendaji ngazi ya vijiji, kata,tarafa na wilaya kwa ujumla waeleweshwe wananchi umuhimu wa reli hiyo.

Ameyasema hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa kawaida wa reli itokayo Arusha hadi Moshi yenye urefu wa zaidi ya kilometa 89 ambayo msafiri ataweza kusafiri kwa kutumia muda wa masaa matatu.

Mhe.Nditiye amesema kuwa lengo la ziara yake ni kujiridhisha na reli hiyo ambapo amewaomba wananchi wa Arusha na Moshi kutambua kuwa reli hiyo ambayo imepatikana na kufufuliwa upya niya watanzania wote hivyo kila mmoja anapaswa kuitunza na kuilinda.

Aidha amesema kwa muda wa zaidi ya miaka 30 kipande hicho cha reli kilikuwa kinaonekana kama ni kitu cha ajabu kutokana na kutokuendelea kwa shughuli za treni katika reli hiyo hivyo kwa kitendo cha kufufua magenge ya ukaguzi wa reli yatakayo kuwa yanafanya kazi ya kusafisha maeneo yote ambayo reli inapita wananchi wanatakiwa kuchukuwa tahadhari zaidi.

"Hakuna treni inayogonga mtu au kitu chochote bali mtu au kitu ndivyo vinaweza kugonga treni hivyo ni muhimu kwa mwananchi kuchukuwa tahadhari mwenyewe kwa kuzingatia alama zitakazowekwa katika vivuko ikiwa ni pamoja na kutoendesha shughuli zozote kandokando ya miundombinu ya treni."Alisisitiza Mhe.Nditiye

Awali katika ziara yake Mhe.Nditiye amewataka wananchi wa Kata ya Lake Tatu Wilayani Arumeru kulinda miundombinu ya reli ambayo inapita katika maeneo yao baada ya kukuta vyuma viwili vilivyokuwa vimewekwa katikati ya reli hiyo ambapo amelielekeza shirika la reli Tanzania kuhakikishi magenge yaliyoko kwenye kipande cha Arusha mpaka Moshi kuanza kufanya kazi ili kuweza kupata mtu anayekagua reli hiyo kabla ya treni kupita.

Vilevile kutokana na hali hiyo amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli za kilimo pembezoni mwa miundombinu ya reli hiyo na kisema kuwa eneo hilo la reli linalindwa kisheria hivyo amewataka wananchi kuanza kujiandaa kisaikolojia kusitisha shughuli za kilimo katika  eneo la reli ili kuweza kutunza miundombinu hiyo na kuweka usalama wa wasafiri.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Moshi Alhaji Mwangi ameliomba shirika hilo kuainisha maeneo ya vivuko kwa kuweka alama na ishara katika njia ya reli ili watu wayafahamu na kuyatumia maeneo hayo kwa usalama zaidi.

Ameongeza kuwa,kwa pamoja wamekubaliana kuimarisha maeneo yaliyopembezoni mwa reli hiyo kwa kuyaacha wazi ambapo wananchi watakayotumia maeneo hayo kwa sasa kwaajili ya kufanya shughuli za kilimo wakishavuna watakuwa wamemaliza shughu za kilimo chao na kwa wale wanaofanya biashara  waendelee huku wakirudi nyuma na kuyaacha wazi maeneo ya reli huku wakihakikisha miundombinu ya reli inakuwa salama wakati wote.

"Viongozi wetu wamejipanga na kukubali kufanya kazi hiyo kwa moyo wa dhati huku wakishirikiana na wananchi ambao ndiyo wanufaikaji wakubwa wa usafiri huu wa reli"Alisema mkuu huyo wa wilaya

Pamoja na hayo mkuu huyo wa wilaya kwa niaba ya wananchi ameliomba shirika hilo kutunza mazingira katika maeneo ambayo yataachwa wazi kusudi yasiweze kugeuka maficho ya wahalifu.

Kwa upande wake Mhandisi Lameki Kamando kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiti Ardhini ameomba shule zote zilizopo karibu na miundombinu ya reli kupewa elimu ya usalama wao kwani kumekuwa na changamoto ya wazazi kuwaacha watoto wao kucheza karibu na reli hiyo.

Sambamba na hayo Kaimu Mkurugenzi wa shitika la reli Tanzania,Focus Makoye ameahidi kuanza mara moja zoezi la utoani elimu kwa wananchi itakayo wawezesha kuchukuwa tahadhari pindi huduma za treni zitakapoanza.
 Naibu waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mhe.Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa viongozi kuhakikisha hakuna mwananchi atakaye endeleza na shughuli za kilimo kandokando ya miundombinu ya reli.
Naibu waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mhe.Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa viongozi wa shirika la reli Tanzania kuhakikisha ukaguzi wa mara kwa mara unafanyika katika njia hiyo ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...