viongozi wa baraza la Chuo hicho wakitoka ndani ya moja ya Handaki litakalopita treni ya kisasa ya umeme (SGR) lililopo Kilosa.
 Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa akifafanua jambo juu ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)  kwa viongozi wa baraza la Chuo hicho walipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa akiangalia reli ya kisasa ( SGR)a inayoendelea kujengwa wakati wa ziara ya viongozi wa baraza la Chuo hicho walipotembelea mradi huo.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji Profesa Zacharia Mganilwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa ziara ya viongozi wa baraza la Chuo hicho walipotembelea mradi wa SGR katika handaki lenye urefu wa zaidi ya kilomita tatu lililopo katika eneo l Mkadege Kilosa Mkoani Morogoro.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
KATIKA jitihada za kupunguza garama za kusomesha wataalamu wa mambo mbali mbali nje ya nchi, chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kushirikiana na Serikali kimesema kitahalakisha kutoa mafunzo kwa wazawa wengi ili kupata wataalamu watakaoweza kujenga reli za kisasa na madaraka makubwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mkuu wa Chuo cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya viongozi wa baraza la chuo hicho ambao walitembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) uliyowafikisha hadi kwenye handaki lenye urefu wa kilomita 1.003ambazo ni sawa na Mita 1131 la kupitia treni ya kisasa ya umeme lililopo Mkadage Kilosa mkoani Morogoro.

Profesa Mganilwa amesema nchi ya Tanzania sasa imefikia katika uchumi wa kati hivyo ni muhimu kuwepo kwa wataalamu wazawa wengi iwezekanavyo watakaoweza kujenga miundombinu ya reli ya kisasa na barabara na ili abiria waweze kufika kwa wakati sehemu waendazo.

"Lengo la ziara yetu ni kuangalia changamoto za rasilimali watu katika miradi mikubwa ya serikali ili tuongeze nguvu katika mafunzo yatakayozalisha wataalamu wa kutosha kwani tukiwa na wataalamu wengi hasa katika sekta za reli bandari na viwanja vya ndege." Amesema Profesa Mganilwa.

Ameongeza kuwa, uzalishaji huo utasaidia wale wenye sifa kupata ajira na kufanya kazi kwa ufanisi pindi tu wamalizapo Masomo yao na wengine baadae kuja kupata leseni za wakandarasi na ikitokea tenda ikatangazwa basi wakandarasi wazawa wataweza kushindana na wale wa nje na utafika wakati tunaweza tusiwe kabisa na wakandarasi kutoka nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa ameishukuru bodi ya NIT kwa kutembelea shirika hilo na kuongeza chuo hicho muhimu katika Shirika hilo kwani wataalamu wengi upande wa usafirishaji waliopo TRC wametokea chuoni hapo. 

Amesema,  zaidi ya trilioni saba zimewekwa katika mradi wa SGR na ili kuwa na reli imara lazima wapatikane wataalamu wa kutosha wa kusimamia sekta hiyo.

"Ili tupate wataalamu hao lazima tuwe na chuo, na NIT ndio Chuo chenyewe hivyo ujio wenu hapa chuoni ni wa manufaa makubwa na ninaamini ushirikiano huu utaendelea," amesema Kadogosa

Meneja Msaidizi wa SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro,  Ayoub Mdachi amesema kwa sasa ujenzi wa SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umefikia asilimia 87 lakini kipande cha Morogoro hadi Makotopola umefikia asilimia 35. kuangalia 

Aidha Mdachi amesema NIT wametembelea mradi huo ili kuangalia namna ambavyo TRC wanasimamia mradi huo mkubwa wa Taifa ili  na wao kama chuo waweze kufanya maamuzi ya kusaidia Serikali katika kutoa wataalamu wa kutosha kwenye sekta hiyo.

Kwa upande wake Mtaalamu na msimamizi wa ujenzi  wa mahandaki ya reli katika mradi wa SGR, kwa kupanda cha Dar es Salaam mpaka Kilosa Hamili Hamis amesema katika mradi huo kuna jumla ya mahandaki manne yenye jumla ya urefu wa mita 2620.

"Maendeleo ya mahandaki haya ni mazuri kwani yote yameshamalizika kuchimbwa na kazi iliyobaki ni kuyajengea zege juu ambapo handaki la pili limeshakamilika kwa asilimia 100 na la pili limeshakamilika kilichobakia ni uwekaji wa kokoto, reli na umeme, katika handaki la kwanza ambalo limekamilika kwa asilimia 98 na tunachomalizia ni kutengeneza njia za wapita kwa miguu huku handaki la tatu tumemaliza uchimbaji sehemu ya juu na la nne nalo limeshachimbwa na tumemwaga zege za chini na kazi ya kuweka nondo kwa ajili ya kumwaga zege inaendelea," amesema Hamis

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...