Waziri wa Madini Doto Biteko akisalimiana nabaadhi ya washiriki katika mgodi wa madini ya Bati wilayani Kyerwa Mkoa waKagera wakati wa ziara yake.
Waziri wa Madini DotoBiteko (katikati) akielekea katika machimbo ya Tin wilayani Kyerwa Mkoa waKagera, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashidi Mwaimu na kushoto ni Afisa
Madini Mkazi wa Mkoa wa Kagera Mhandisi Lucas Mlekwa.






Waziri wa Madini Doto Biteko akitazama machimboya Madini ya Bati (Tin) alipofanya ziara yake ya kikazi wilayani Kyerwa Mkoa waKagera


Waziri wa Madini Doto Biteko akitazama machimboya Madini ya Bati (Tin) alipofanya ziara yake ya kikazi wilayani Kyerwa Mkoa waKagera
Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati)akielekea katika machimbo ya Tin wilayani Kyerwa Mkoa wa Kagera, kulia ni Mkuuwa Wilaya ya Kyerwa Rashidi Mwaimu na kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa waKagera Mhandisi Lucas Mlekwa
Waziri wa Madini Doto Biteko akikagua vifaavinavyotumika kuyeyushia Madini ya Bati mara baada ya kufanya ziara yake yakikazi wilayani Kyerwa Mkoa wa Kagera.
WAZIRIwa Madini Doto Biteko kushoto akisalimiana na mchimbaji mdogo wa madini
ya bati (TIN) katika soko la madini Kyerwa mara baada ya kumalizamkutano nao
WAZIRIwa Madini Doto Biteko akitoa kwenye ukumbi wa mikutano wa soko la
madini ya bati(TIN) Kyerwa mara baada ya kumaliza mkutano na wachimbaji
wa madini hayo



Na Tito Mselem Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli anataka wachimbaji wote wa madini nchini wafaidike na madini
ambayo Mwenyezi Mungu amewabariki kuwanayo katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko, alipokuwa
kwenye ziara yake ya kikazi wilayani Kyerwa Mkoa wa Kagera ambapo
alizungumza na wachimbaji pamoja na wafanyabiashara wa Madini ya Bati
(Tin).

Waziri Biteko alisema, anachokitaka Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ni kuona wachimbaji wote wa madini nchini wanafaidika na madini
yaliyopo kwenye maeneo yao, hii ndiyo awamu ya wachimmbaji kutajirika.

“Wote ni mashahidi kwa muda mrefu madini yetu yalikuwa
yanatoroshwa, lakini Mheshimiwa Rais akasema hapana tuanzishe masoko,
leo wote tunaona mafanikio makubwa yanayotokana na masoko hayo,” alisema
Waziri Biteko.

Tanzania hatukuwahi kuwa na Cheti cha Uhalisia wa Madini ya
Bati lakini Rais akasema hapana tutafute Cheti cha Uhalisia lakini
tunashukuru Mungu Cheti cha Uhalisia tumekipata, Biteko aliongeza.

Aidha, Waziri Biteko amewaruhusu wafanyabiashara wa Madini
ya Bati kuyasafirisha madini yaliyoongezwa thamani kwenda kuuzwa nje ya
nchi ili yauzwe kwa bei nzuri na wachimbaji kufaidika.

Pamoja na mambo mengine Waziri Biteko, amewataka wachimbaji
wa Madini ya Bati kurejea kazini na kuachana na vitendo vya kutorosha
madini hayo na badala yake wayapeleke sokoni.

Pia, Waziri Biteko amewataka wachimbaji hao kupendana,
kuthaminiana na kuachana na mambo ya majungu ili kujikita katika
kuongeza tija kwenye shughuli yao ya uchimbaji madini.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashidi Mwaimu
alimpongeza Waziri wa Madini, kwa kazi nzuri anazozifanya na kuwataka
wachimbaji wa Madini ya Tin kutumia fursa hiyo kueleza changamoto zao
mbele ya Waziri.

Nae, Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa Madini ya Tin
wilayani Kyerwa Osward Inyasi, kwa niaba ya wachimbaji wenzake alieleza
kuwa wachimbaji wa madini ya Tin bado wanashida ya wanunuzi wa madini
yao kwani hadi sasa wana zaidi ya tani 20 zimewekwa stoo baada ya kukosa
wanunuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...