RAIA sita wa China wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuongoza genge la uhalifu na kukutwa na nyara za serikali.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na wakili wa serikali Salim Msemo akisaidiana na wakili Eliya Athanas  imewataja washtakiwa hao kuwa ni, Jin Erhao (35) anayejishughulisha na shughuli za usafirishaji, Chengfa Yang (49) mfanyabiashara, Ren Yuangqing (55) Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji ya Sinota, Shu Nan (50) mfanyakazi katika kampuni hiyo, Chen Shinguang (45) Meneja katika kampuni hiyo na Gu Jugen (57) Meneja ufundi wa kampuni hiyo wote wakiwa ni wakazi wa mtaa wa Sokoine, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabate imedaiwa, Agosti mosi, 2020 katika mtaa wa Sokoine, Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa wote kwa pamoja na kwa makusudi walisimamia genge la uhalifu lililopelekea kupatikana kwa ndege aina ya Tausi mwenye thamani ya USD 500 sawa na Sh 1,155,000 za Tanzania kinyume cha sheria ya wanyama pori.

Katika shtaka la pili washtakiwa hao wanadaiwa Agosti Mosi, 2020 katika mtaa wa  Sokoine  jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walikutwa na nyara ya serikali ambayo ni Tausi mmoja mwenye thamani ya Sh 1,155,000/- kinyume na sheria ya wanyama pori.


Pia washtakiwa hao wanadaiwa, Agosti Mosi, 2020 katika mtaa wa Sokoine, Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa walikutwa na nyara za serikali ambayo ni ndege aina ya Tausi mmoja mwenye thamani ya Sh 1,155,000/-

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, wakili Msemo alidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na hawana  pingamizi la dhamana lakini waliomba masharti yawe makali kulingana na mashtaka yalivyo.

Akisoma masharti ya dhamana hakimu Kabate amewataka washtakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika walio ndani ya Mamlaka ya Mahakama (Ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani) watakaosaini Bondi ya Sh 500,000 Kila mmoja na kuwasilisha pasi zao za kusafiria Mahakamani. Pia washtakiwa wameamriwa  na kuwapa amri ya kutokusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama.

Wakili wa utetez ibrahimui Bendera alidai Mahakamani hapo kuwa pasi za kusafiria za washtakiwa hao kwa Sasa zinashikiliwa na Polisi hivyo uwezekano wa kuziwasilisha kwa wakati ule haukuwepo ambapo Hakimu Kabate alimtaka kuwasilisha uthibitisho iwapo ni kweli pasi hizo ziko mikononi mwa Polisi.

Aidha amewataka mawakili wa pande zote kushirikiana kupata uthibitisho huo ili waweze kuwapatia washtakiwa dhamana.

"Wakili Msemo mnaweza kushirikiana kupata uthibitisho, hata kwa simu, Mimi nipo mkipata uthibitisho tutakamilisha dhamana lakini kwa Sasa washtakiwa watabaki mahabusu mpaka tupate uthibitisho" alisema Hakimu Kabate.

Kufuatia hayo, washtakiwa wamerudishwa rumande hadi Agosti 20,2020 kesi hiyo itakapotjwa tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...