Na Zainab Nyamka, Michuzi TV.

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakar Kunenge amewaagiza Mamlaka ya Majjsafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha wanapeleka miradi mikubwa ya maji katika maeneo yenye wakazi wengi.

Akizungumza na Menejimenti nzima ya Mamlaka hiyo ikiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Cyprian Luhemeja, amesema kuwa Dawasa wanatakiwa wasijilinganishe na taasisi zingine bali wanatakiwa wafike kimataifa.

Kunenge amesema, naifahamu Dawasa kwani nilishakua hapa wakati wa dawasco nafahamu changamoto zilizokuwa zinakuta ila kwa sasa  
mkoa wa Dar  es Salaam mmejitahid na mmefanya kaz kubwa na ni miongoni mwa taasisi zilizofanya kazi vizuri.

"Nilifanya ziara maeneo ya Pugu, wananchi walitoa malalamiko katika sekta ya maji ila mwakilishi wenu kutoka Kisarawe alielelezea kuna mradi kutoka Kisarawe hadi Pugu wananch walifarijika sana," amesema Kunenge.

Amesema, Dawasa wana kazi kubwa ya kufanya ikiwemo kutoa taarifa kwa wananchi wafahamu mradi umefikia wapi na lini utakamilika ili kutatua changamoto ya maji.

"Najua mmejipanga vizuri, miradi hiyo inayotekelezwa iondoe changamoto kwa wananchi na mhakikishe hadi kufikia wakati wa uchaguzi changamoto ziwe zimekamilika,"amesema

Kunenge amesisitiza kuwa,  Dawasa hawafanyi Biashara ila wanatoa huduma kwa wananchi na mnapopata mapato mengi basi fedha hizo zinaenda katika uwekezaji wa miradi hususani kwenye maeneo yanayoendelea kukua kwa kasi.

"Maeneo ya Kigamboni na Mwabepande, ni maeneo ambayo yanaendelea kukua zaidi kwani mkakati wa serikali ni kuona mkoa wa Dar  es salaam unakuwa mkoa wa uwekezaji" amesema.

"Nafarijika nasikia nchi nzima wanatumia kauli ya mtue mama ndok kichwani kwan najua ilianzia hapa na mnatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya kutatua changamoto ya maji",

Mkuu wa Mkoa ahadi ya kutembelea miradi yote ya Dawasa pamoja na kutembelea maeneo yenye changamoto kubwa ya maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, ametoa pongezi kwa Mtendaji Mkuu wa Dawasa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutekeleza miradi ya Dasawa kwa fedha Za ndani tofauti na zamani ambapo walikuwa wanasakamwa kwa madeni makubwa.

Naye Mtendaji Mkuu, Mhandisi Luhemeja amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuja kuwatembelea pamoja na kutoa maagizo yake ambapo wameahidj kuyatekeleza kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abuubakar Kunenge akizungumza na wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA baada ya kuwatembelea katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa taarifa fupi ya miradi inayotekelezwa na Mamlaka hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abuubakar Kunenge baada ya kuwatembelea katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.
 Wakurugenzi mbalimbali wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abuubakar Kunenge baada ya kuwatembelea katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...