Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akihutubia katika kilele cha Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa akihutubia wakati wa kilele cha maonesho hayo. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Nchimbi.


Na Richard Mwaikenda, Dodoma

VIONGOZI wa mikoa ya Singida na Dodoma wameiomba Serikali kulikubali ombi lao la Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kitaifa mwaka 2021, yafanyike Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Kauli hiyo aliitoa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi wakati wa hafla ya kufunga rasmi Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yaliyofanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Stella Ikupa kwenya viwanja hivyo.

Akihutubia katika kilele cha maonesho hayo, mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu) Stella Ikupa, Dk. Nchimbi alisema kuwa tayari ombi hilo lilishatumwa serikalini. Waziri Ikupa alijibu kuwa watalifanyia kazi ombi hilo.

Dk. Nchimbi alitaja sababu tatu za kuomba maonesho hayo kufanyika kwenye kanda hiyo kuwa ni; Kuwashukuru wananchi kuchagua viongozi bora kama kauli mbiu ya maonesho hayo wakulima, wafugaji na wavuvi inavyosema kuwa Chagua Viongozi Bora.

Alisema kuwa anaamini bila wasiwasi wowote kuwa Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli atashinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo itakuwa ni sherehe kubwa kufanyika Dodoma na kutimiza kauli mbiu ya Maonesho Nanenane ya mwaka huu. Maonesho ya Kanda Kati yanashirikisha mikoa ya Singida na Dodoma.

Sababu nyingine ni kumshukuru Mungu kutuondolea nchini ugonjwa hatari wa Corona hasa baada ya Rais John Magufuli kuwaomba viongozi wa dini zote, wasio na dini pamoja na wananchi kwa ujumla kumuomba Mungu kwa siku awaepushe na ugonjwa huo, tamko ambalo lilitolewa mkoani Dodoma.

Tatu ni kusherehekea Makao Makuu ya Nchi kuwa Dodoma ambayo ipo Kanda ya Kati, kwani hadi sasa ni miaka mitatu imepita tangu Rais John Magufuli atangaze rasmi mwaka 2017, haijawahi fanyika sherehe ya shukrani kwa jambo hilo muhimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...