*****************************

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameanza ziara ya kukagua na kufuatilia ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa kata zote za Tarafa ya Mihambwe ambapo ameridhishwa na ujenzi na ukamilifu wa miradi ya ujenzi ya nyumba ya Mwalimu pamoja na vyoo shule ya Msingi Mpunda iliyopo Kijiji cha Mpunda kata ya Michenjele.

Hayo yamejidhihirisha kwenye ziara hiyo aliyoifanya Gavana Shilatu ambapo amefurahishwa na ubora wa miradi hiyo ambayo pia imekamilika kwa wakati.

“Kazi kubwa imefanyika, ni ngumu kuamini leo hii kwa mara ya kwanza Kijiji cha Mpunda wanakuwa na nyumba ya kisasa ya kuishi ya Mwalimu pamoja na vyoo vya kisasa vya Wanafunzi na Walimu. Shukrani kwa Rais Magufuli kwa kutupatia fedha takribani Tsh. Milioni 37. Nawasisitiza kuitunza miradi hii idumu kwa manufaa ya nyakati zote.” Alisisitiza Gavana Shilatu.

Nae Mwalimu Seleman Seleman ameshindwa kuzuia hisia zake kwa Rais Magufuli ambaye amewezeshwa ukamilifu wa miradi hiyo.

“Miradi yote ya nyumba na vyoo imekamilika kwa asilimia 100, kiukweli tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kutujali Watumishi hususani Waalimu kwa kutoa fedha za kujengea nyumba hii.” Alisema Mwalimu Seleman.

Mradi wa nyumba ya Mwalimu umegharimu Tsh. Milioni 33.5 na ukarabati wa vyoo kwa Tsh. 3.5 na miradi yote imeshakamilika kwa asilimia 100 tayari kwa matumizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...