Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akikagua mojawapo ya mabanda ya wajasiriamali waliojitokeza kwenye siku ya kupinga biashara haramu jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya upingaji biashara haramu jijini Dodoma.

SERIKALI imetoa rai kwa watanzania wote wanaoishi nje ya nchi kuzingatia taratibu za kisheria zenye lengo la kuwalinda pamoja na kupata hati za kusafiri nje ya nchi.

Amesema hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya kupinga biashara haramu ya usafirisha wa binadamu duniani, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema kuwa hakuna haja ya watanzania kurubuniwa na watu wenye nia mbaya wanaojitangaza kuwa na uwezo wa kuwatafutia kazi nje ya nchi au ndani ya nchi bali utaratibu wa serikali ufuatwe.

"Utaratibu rahisi ni kibali cha mzazi na serikali ya kijiji, anapotoka kuja mjini tunaweza tukajua na kumlinda katika kuangalia haki zake na kuangalia endapo atapata madhara yoyote, cha kushangaza watu wanaofanya kazi hiyo hawataki kufuata taratibu za kisheria ambazo zimewekwa na serikali.’’ Amesema Waziri Simbachawene.

Waziri Simbachawene amewataka majirani, wanaposikia manyanyaso katika familia fulani kwa mtoto ambae siyo wa familia hiyo ni vema wakatoa taarifa kwenye kituo cha Polisi au uongozi wa mamlaka za serikali.

Pia ameongeza kuwa wapo watanzania walioenda nje ya nchi kama Dubai na kwingineko kwa kufuata utaratibu uliopo ikiwa ni pamoja na kujaza mikataba ya ajira ambayo imethibitishwa na ofisi za balozi za Tanzania pamoja na wizara zinazohusika na ajira hapa Nchini.

‘’Waliowengi wapo salama huko waliko na hawapati mateso ya aina yoyote kwaiyo ukifuata utaratibu kimsingi maisha hata huko uliko yanakua salama.’’ Amesema Simbachawene.

Aidhaa Waziri Simbachawene amesema kuwa itifaki ya kimataifa ya mwaka 2000 ilifikiwa na ilikua na madhumuni matatu makuu, ikiwemo kuzuia na kupinga usafirishaji haramu wa binadamu hususani wanawake na watoto, pili kuwalinda na kuwatetea wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji  wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuheshimu haki zao pamoja na kukuza na kuhamasisha ushirikiano miongoni mwa Nchi wanachama ili kufikia malengo ya kuzuia na kupambana na biashara haramu.

Nae mwakilishi kutoka shirika la kulinda na kutetea haki za watoto Nchini, SAVE THE CHILDREN amesema shirika lao limeanzisha miradi maeneo mbalimbali ikiwemo Zanzibar pamoja na mikoa ya  Iringa, Dodoma, Rukwa, Morogoro, Kigoma na Kasulu lengo likiwa kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi pamoja na kupinga ukatili wa aina yoyote ile ikiwemo biashara ya binadamu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kuzuia na kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu, Adatus Magere amesema kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania iliadhimisha siku hiyo mwaka 2019, ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau ilifanya mambo mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari, kutoa ushauri bure wa kisheria kwa wahanga wa biashara haramu ya binadamu pamoja na kufanya kongamano la kitaifa kuhusu biashara haramu ya biandamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...