WANAHABARI nchini wametakiwa kutumia taaluma yao vizuri katika kuikumbusha jamii kuwa na uwajibu katika kuwawezesha wazazi kufanikisha unyonyeshaji ili kuboresha hali ya lishe ya watoto na kuendeleza nguvu kazi yenye tija kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina  ya siku moja ya wanahabari, Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Bi Sikitu Simon Kihinga, amesema kuwa vizuri kuyatumia vyema yale watakayojifunza ili kuendelea kutoa taarifa sahihi na kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya lishe.

Bi. Kihinga amesema kuwa semina hiyo kwa wanahabari imelenga kuzungumzia maadhimisho wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama duniani kwa mwaka huu, ambapo kuanzia Agosti 1 hadi 7 kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyengine duniania kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama.

Ameeleza kuwa maadhimisho hayo ni fursa ya pekee katika kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali na jamii ili kufikia malengo ya kulinda, kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

"Mama anatakiwa kunyonyesha mtoto maziwa saa moja ya kwanza mara tu baada ya kujifungua pamoja na kuhakikisha mtoto anaendelea kunyonya mara kwa mara kadiri ya uhitaji wake bila kupangiwa ratiba" amesema Bi. Kihinga.

Amefafanua kuwa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani kwa mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu "Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na ulinzi wa mazingira".
Ameeleza kuwa kauli hiyo imelenga kuwakumbusha mchango wa unyonyeshaji katika utunzaji wa mazingira ya dunia pamoja na kulinda afya.

"Jamii inatakiwa kuendelea na juhudi za kulinda, kuhimiza na kuendeleza na unyonyeshaji watoto maziwa ya mama kama njia mojawapo ya kupata matokeo chanya" amesema Bi. Kihinga.
Bi. Kihinga amebainisha kuwa takwimu za hali ya ulishaji watoto nchini zinaonesha takribani asilimia 97  ya watoto wenye umri mdogo chini ya miaka miwili wananyonyeshwa na maziwa ya mama.

Amesema idadi ya watoto wanaoanzishwa vyakula vya nyongeza kwa wakati sahihi katika umri wa miezi 6 hadi 8 ni asilimia 87, wakati idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6-23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni asilimia 35.

Ameeleza kuwa ni muhimu kuendelea kukumbusha wajibu wa makundi mbalimbali ya wadau wa lishe kusaidia na kuondoa vikwazo vinavyochangia baadhi ya wanawake kushindwa kunyonyesha watoto wao kikamilifu.

Bi. Kihings amesema jamii inaitaji kutambua kuwa ili kuendelea usalama wa dunia na kizazi kijacho tunahitaji hatua za haraka ili kulea malenzi mazuri kwa mama kutokana unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni suluhisho majawapo ambalo linahitaji ushiriki mkubwa wa sekta mbalimbali ili kutatua changamoto.

Katika semina hiyo wanahabari wamefundishwa mada mbalimbali ikiwemo Afya ya lishe vijana balehe, Mama mjamzito na anayenyonyesha, ulishaji wa watoto wachanga kabla ya kutimiza meiezi sita, ulishaji wa watoto vyakula vya nyongeza (baada ya mienzi 6)
Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Bi Sikitu Simon Kihinga (kushoto) akiwafundisha waandishi wa habari dhana ya wiki ya unyonyeshaji Tanzania leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Afisa lishe mtafiti idara ya elimu na mafunzo ya lishe, taasisi ya chakula na lishe tanzania, bw. Walbert mgeni akitoa ufafanuzi wakati wa semina ya siku moja ya wanahabari leo jijini dar es salaam kuhusu umuhimu mama kunyonyesha mtoto.
(Picha na emmanuel massaka wa michuzi TV)
Afisa mawasiliano taasisi ya chakula na
lishe tanzania.,
Jackson Monela akiwagawia waandishi wa habari Kitini cha Lishe ya Wanawake
Watoto  na Vijana Barehe  
wakati wa  semina ya siku
moja ya wanahabari
 leo jijini dar es salaam.

Waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti vya habari wakiwa katika semina leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Bi Sikitu Simon Kihinga (alie simama) akifunga semina hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...