*Dkt. Akwilapo awataka wakaguzi na wahasibu kupiga kazi kwa ufanisi 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema mafunzo yanayotolewa kwa wahasibu na wakaguzi yanatakiwa kuleta matokeo ya ufanisi katika kutatua changamoto mbalimbali. kutokana na mada ambazo zimewasishwa na wararibu wa mafunzo.

Hayo aliyasema  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonald  Akwilapo  wakati akifunga mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam,  

Dkt  Akwilapo  amesema kuwa mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yanatakiwa kuleta matokeo katika wizara kwa kupunguza  mzunguko taarifa katika masuala ya uhasibu na ukaguzi.

Amesema TIA ni wabobezi hivyo fedha ya serikali inatakiwa  kusimamiwa  hasa katika miradi ya ujenzi ambapo kuna baadhi ya sehemu haijafanyika viziuri  hivyo kunahitaji kufatilia kwa ukaribu miradi mbalimbali ya ujenzi.

Dkt.Akwilapo amesema mafunzo hayo ykuondoa hoja za ukaguzi katika wizara kwa kuendelea  kuwa  wasimamizi ambapo hadi sasa tumekuwa tukifanya vizuri katika wizara tatu ambazo zimekuwa  na mafanikio ikiwemo wizara ya elimu,Sayansi na Teknolojia .

Amesema kuwa fedha inayotolewa na serikali katika bajeti au fedha inayotoka vyanzo vya ndani  zinatakiwa kusimamiwa katika mipango iliyokusudiawa.

"Mafunzo  yanalenga kuimarisha katika  usimamizi wa fedha  ya serikali hivyo ushiriki wenu wataalam katika masuala haya yatafanya  wizara kuendelea kufanya vizuri zaidi "amesema Dkt. Akwilapo.

Aidha amesema  mada zilizotolewa zimegusa  maeneo mbalimbali yalikuwa na changamoto hivyo mada hizo zitakuwa zimewajenga kwa kwenda kuwa na utofauti katika utendaji wenu wa kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Wizara hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilamali Watu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Moshi Kabengwe  akizungumza kuhusiana na mafunzo na namna yatavyoleta ufanisi katika wizara hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Mafunzo wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) George Kasinga  akizungumza na  Wahasibu na Wakaguzi wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia wakati kufunga mafunzo wa hizo ,jijini Dar es Salaam.
 Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekonolojia Anna Mhere akitoa shukrani kwa mgeni rasmi kuhusiana na mafunzo waliyoyapata.
 Baadhi ya Wahasibu na Wakaguzi wakiwa katika mafunzo.
 Baadhi ya wakaguzi na wahasibu wakiwa katika mafunzo.
Picha ya Pamoja Wahasibu na Wakaguzi na  Mgeni Rasimi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo mara baada ya kufunga mafunzo. 
Katibu Mkuu wa Wizara ye Elimu ,Sayansi na Teknolojia akiwa katika picha ya pamoja na kamati iliyoandaa mafunzo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...