Na Woinde Shizza, Michuzi TV  Arusha

VIONGOZI wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha wanatekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli ya kuhakikisha usafiri wa treni unafika katika Mkoa wa Arusha kwa usalama.

Hayo yalibainishwa na  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maofisa Tawala,Maofisa Tarafa na wenyeviti wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Wilaya ya Arumeru.

Amesma maono ya Rais ni kuhakikisha treni inafika Arusha mwishoni mwa Agosti ili isaidie sekta ya usafirishaji na kuokoa muda wa wananchi kusafiri muda mrefu.

"Ni miaka 30 imepita tangu treni ifike mkoani Arusha,hivyo wananchi tunatakiwa kufurahi na kuipokea kwa moyo mkunjufu,"amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa ajali kutoka Shirika la Reli Tanzania  Maizo Mgedzi amesema, wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari hasa kipindi ambacho treni itaanza kufanya kazi hasa wanaofanya shughuli mbalimbali karibu na reli.

Amesema ni hatari kufanya shughuli mbalimbali za kibinadamu karibu na reli kama kulima, kupitisha Wanyama,kuegesha Pikipiki na Magari,kuwa na Viwanja au kujenga karibu na reli na kwamba treni inaenda kuwa msaada mkubwa kwani itakuwa inaleta malighafi mbalimbali kwa ajili ya viwanda vilivyopo Arusha na hata kwa wafanyabiashara.

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta, alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa tawala,Maafisa Tarafa na wenyeviti wa halmashauri ya jiji la Arusha na wilaya ya Arumeru Juzi katika ukumbi wa mikutano was jengo la halmashauri ya Meru(picha na Woinde Shizza)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...