Na Amiri Kilagalila,Njombe

Waandishi wa habari mkoani Njombe wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona (Covid-19) vinavyosababisha homa kali ya mapafu,pindi wanapo kuwa katika majukumu yao ya kazi pamoja na kuendelea kuhabarisha umma kuendelea kuchukua tahadhari hiyo.

Licha Taifa la Tanzania kuwa salama dhidi ya virusi vya Corona kutokana na kuondolewa hofu ya virusi hivyo,wito umetolewa na Bi,Eveline Kidenya afisa afya wilaya ya Njombe kwa makundi mbalimbali likiwemo kundi la waandishi wa habari kuendelea kuchukua tahadhari hasa pindi wanapokuwa katika mikusanyiko.

“Tuwe huru,tuishi na kirusi hicho kama tunavyoishi na virusi wengine au Bakteria wengine,cha msingi tusipuuzie kuendelea kuchukua tahadhari tunapokutana na wageni ambao sio wana Njombe kwa kuwa kama Njombe tuko salama tusifikiri na watu wa maeneo mengine wako salama”alisema Bi Eveline Kidenya

Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania kwaufadhili wa nchi ya sweedeni kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe NPC wametoa mafunzo hayo dhidi ya kujikinga na Corona kwa waandishi wa habari wanachama kupitia wataalamu wa afya ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya Njombe.

“Tumepata mafunzo haya ambayo yapo katika mpango mkakati wa UTPC umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania wakipata ufadhili kutoka ubalozi wa Sweeden kwa ajili ya kutuwezesha waandishi wa habari kutoa habari lakini vile vile kujikinga na maambukizi haya ya Corona”alisema Hamis Kassapa katibu wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe NPC

Erasto Mgeni na Emiria Msafiri ni baahi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika semina hiyo wamesema wamepokea vema mafunzo hayo huku wakiadhi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kundelea kuchukua tahadhari ili kujikinga na virusi hivyo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Njombe,wawakilishi kutoka vyombo mbambali vya habari nchini Tanzania wakati wakikumbushwa mambo mbali mbali juu ya magonjwa ya mlipuko hususani mambukizi ya virusi vya Corona katika semina iliyofanyika hii leo ukumbi wa Dosmeza mjini Njombe.
 Bi,Eveline Kidenya afisa afya wilaya ya Njombe wakati akitoa maelekezo juu ya magonjwa ya mlipuko na virusi vya Corona.
 Katibu wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe NPC Ndugu Hamis Hassan Kasapa akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa semina ya siku moja juu ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya milipuko hususani Corona.
 Waandishi wa habari mkoa wa Njombe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya semina ya kuelimishana namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa ya milipuko hususani ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...