Na Karama Kenyunko, Michuzi TV



Wafanyabiashara wawili wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi nyenye mashtaka ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuongoza genge la uhalifu.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Agosti 10,20202 na wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon imewataja washtakiwa hao kuwa ni Mohamed Mkumba maarufu kwa jina la Muddy (32) Mkazi wa Kitunda Mwanagati na Karume Karume (48) anayeishi Mbagala Kokoto.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Yusto Ruboroga imedaiwa kuwa, Julai 24, 2020 huku Kitunda Mwanagati  washtakiwa walisafirisha gramu 25.24 za dawa za kulevya aina ya Heroine

Pia imedaiwa, kati ya Juni 2019 na Julai 2020 jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa kushirikiana na wengine ambao bado hawajakamatwa walishiriki kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine kinyume na sheria

Hata hivyo washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Agosti 28, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Washtakiwa wamerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...