:Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles


 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa fomu za uteuzi kwa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa vyama kumi na sita (16) vya siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo tarehe 11 Agosti 2020, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Dkt. Wilson Mahera Charles amesema fomu kwa wagombea hao zimetolewa kuanzia tarehe 5 Agosti 2020.

Dkt. Mahera amesema kwamba wagombea hao wanatarajiwa kurejesha fomu hizo tarehe 25 Agosti 2020 kwa ajili ya uteuzi ambao utafanyika siku hiyo.

Amewataja wagombea ambao wamechukua fomu mpaka sasa kwamba ni pamoja na Seif Maalim Seif na Rashid Ligania Rai (AAFP), Philipo John Fumbo na Zaina Juma Hamisi (DP), Leopold Lucas Mahona na Khamis Ali Hassan (NRA) na John Pombe Joseph Magufuli na Samia Suluhu
Hassan (CCM).

Wengine ni Muttamwega Bhatt Mgaywa na Satia Mussa Bebwa (SAU), Queen Cuthbert Sendiga na Shoka Kamis Juma (ADC), Twalib Ibrahim Kadege na Ramadhani Ali Abdallah (UPDP), Bernard Kamilius Membe na Omar Fakih Hamad (ACT Wazalenda), Cecilia Augustino Mmanga
na Tabu Mussa Juma (Demokrasia Makini) na Tundu Antiphas Lissu na Salum Mwalim Juma Mwalimu (CHADEMA).

Amewataja wengine kuwa ni Hashim Rungwe Spunda na Mohammed Massoud Rashid (CHAUMMA), Khalfani Mohammed Mazrui na Mashavu Ulawi Haji (UMD), David Daud Mwaijojele na Ali Said Juma (CCK), Ibrahim Haruna Lipumba na Hamida Abdalla Huweishil na Haji Ambari Khamis (NCCR Mageuzi) na John Paul Shibuda na Hassan Kornely Kijogoo (ADA-
TADEA).

Dkt. Mahera amesema kwamba chama NLD ambacho kilionesha nia ya kuchukua fomu kimeiarifu Tume kwamba bado hakijafanya uteuzi wa wagombea, hivyo Tume itaweka utaratibu wa kutoa fomu kwa wagombea wa chama hicho watakapokuwa tayari ndani ya kipindi hiki cha
utoaji wa fomu za uteuzi.

Imetolewa na:
Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...