Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
 WAKAZI sita wa Kijiji cha Mpeta, Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wamemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa awasaidie walipwe fedha zao kiasi cha Sh.milioni 15, ambazo ni gharama walizotumia kuleta amani katika kijiji hicho kutokana na mapigano ya askari na wananchi yaliyotokea Oktoba 16 na 17,2015.

Pia, walifanikisha kupatikana kwa silaha mbili za Jeshi la Polisi (Bastola na SMG) ambazo zilipotea katika mapigano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wenzake watano, Gerald Ibrahim maarufu kwa jina la Serikali ambaye ndiye aliyeongoza kupatikana kwa silaha hizo na kupatikana kwa amani kijijini hapo amesema, baada ya tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma walikaa kikao ndipo Katibu Tarafa wa Nguruka aliniambia kuwa amepata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa yeye unaweza kusaidia kupatikana kwa hizo silaha, kuzuia ghasia na kuleta amani. 

Amesema, alikubali kufanya kazi hiyo iliyokuwa ikimgharimu Sh.Milioni 15 ambayo mpaka leo hajalipwa chochote...,  "kazi ilifanyika kubwa nilitawanya vikosi vya vurugu na kufanikiwa kupata silaha zilizopotea lakini mpaka sasa sijaalikwa kitu".

"Ni miaka mitatu sasa tangu mwaka 2018 nilipopewa kazi na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Mkoa, nilitumia fedha hizo kufanikisha upatikanaji wa silaha na kweli  zilipatikana, namwomba Waziri Mkuu anisaidie nilikopa pesa hizo kutoka kwa watu mbalimbali  na sasa wananidai." Amesema serikali.

Ameeleza chanzo za madai kuwa, Oktoba 16 na 17, 2018 yalitokea mapigano kati ya wananchi wa kijiji hicho na Askari Polisi na katika mapigano hayo zilipotea silaha mbili hali iliyosababisha uongozi wa Mkoa na Wilaya kumtuma kufanya kazi hiyo kutokana na kukubalika na wananchi.

"Nilifanikiwa kutuliza ghasia, tuliitafuta  silaha tukafanikiwa kuzipata na kuzikabidhi kwa uongozi wa wilaya, niliandika maombi ya kulipwa fedha" alisema Serikali.

"Tunamuomba Waziri Mkuu atusaidie tulipwe fedha zetu kwa sababu, tulitumia gharama zetu kufanikisha kuleta amani na kupatikana kwa silaha".Amesema Ibrahimu.
Mfanyabiashara, Gerlad Ibrahimu maarufu kama 'Serikali' akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...