Na Woinde Shizza,ARUSHA

WANANCHI  wote wanaotembelea Maonesha ya wakulima (Nanenane) wametakiwa kuyafanyia kazi yale yote wanaojifunza katika maonyesho hayo  kwani mafunzo hayo yanaweza kubadilisha maisha yao kwa ujumla .

 Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC)Kanda ya Laskazini  Lewis Nzari Mtei wakati akizungumza na vyombo vya habari katika  maonyesho ya 27 ya wakulima yanayofanyika viwanja vya Themi Njiro Nane nane mkoani Arusha.

Ameeleza kuwa ni vyema kila mwananchi ambaye anaenda  kutembelea maonyesho hayo akajifunze  kwa vitendo huku akizingatia masuala ya mazingira.Amebainisha kauli mbiu ya maonyesha hayo kwa mwaka huu inasema   kwa maendeleo ya kilimo ,uvuvi, ufugaji   chagua  viongozi bora 2020  inagusa kila upande.

Na kwamba inasisitiza zaidi kuchagua viongozi bora ambao wanaweza kuhamasisha  vyote vilivyotaja ambapo alisema kuwa katika vyote hivyo vinategemeana   na suala zima la mazingira

Amesema  suala la kilimo linategema mazingira iwapo kutakuwa na mazingira mazuri basi hata mkulima ataweza kuvuna mazao mengi wakati katika ufugaji unategemea mazingira maana hakuna mfugaji atafuga katika mazingira mabovu, hivyo ni wajibu wa kila mtu kulinda mazingira ili aweze kufaidika na kile anacho kifanya.

Aidha ameataka wananchi wa kanda ya kaskazini  kuwekeza katika ufugaji wa samaki kwani ufugaji huu ni mzuri sana na hauaribu mazingira ,hivyo ni vyema wananchi kutembelea  wataalam ambao  wanahusika na swala la ufugaji wa samaki ili kupata elimu zaidi na kuchukuwa hatua juu ya ufugaji wa zao hilo kwani linafaida kubwa na alitumii gharama kubwa .

Amewasisitiza wananchi kuendelea kutunza mazingira yao kwani ndio maisha yao  huku akiendelea kusisitiza kuacha kutumia mifuko ya plastiki na kuwasihi kuendelea kutumia mifuko mbadala ambayo kwa sasa hivi ipo kla mahali

"Katika kipindi hichi cha Nane nane tupo hapa na tutaendela kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mazingira,hivyo niwaombe wananchi waje kwa wingi katika banda letu ili waje wapate elimu nzuri kuhusu mazingira,"amesema Mtei.
Meneja wa Baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC)kanda ya kaskazini Lewis Nzari Mtei wakati akiongea waandishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...