Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Imeelezwa kuwa kumekuwa na ongezeko  la watoto wenye umri wa miaka 7 hadi 16 wanaojua kusoma, kuhesabu na kuandika (KKK) katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

Hayo yamesemwa katika uzinduzi wa tathmini kwa wa watoto wanaojua KKK  uliofanywa na  taasisi ya Uwezo kwa watoto 58530 nchini ambapo wilaya ya Ludewa ilishika nafasi ya 16 kitaifa.

Awali wilaya hiyo ilishika nafasi ya 56 kitaifa na kuonyesha kuwa kwan sasa imezidi kupanda kiwango. 

Katika uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu ambapo mgeni rasmi alikuwa katibu Tawala wa wilaya ya Ludewa.

 Katibu tawala wilaya ya Ludewa Zainabu Mlawa akipokea ripoti ya tathmini iliyofanywa na Uwezo juu ya watoto wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kimbila na Ludewa mjini waliohudhulia uzinduzi wa ripoti ya watoto wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK)

 Katibu tawala wilaya ya Ludewa Zainabu Mlawa akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa elimu na wanafunzi baada ya uzinduzi wa ripoti ya watoto wanaojua kusoma, kuhesabu na kuandika ( KKK)
 Wanafunzi, wazazi pamoja na wadau wa elimu wakifuatilia uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya wanafunzi wanaojua kusoma , kuhesabu na kuandika ( KKK).
 Baadhi ya viongzi waliohudhuria uzinduzi wa ripoti ya watoto wanaojua kusoma, kuhesabu na kuandika (KKK) Kutoka kushoto ni Mratibu wa Uwezo wilaya ya Ludewa Lenis Mtitu, Katibu tawala wilaya ya Ludewa Zainabu Mlawa, Afisa taaluma wilaya ya Ludewa Blandina Mlelwa na Mwl. Florian Mtweve

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...