Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya Edward Mbanga akiongea na Wauguzi Wakuu wa Wilaya nchini wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji kazi kwenye ukumbi wa Cathedral jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu akiongea na viongozi hao wakati wa kikao cha mafunzo ambapo aliwataka kuweka dhamira na malengo ya dhati katika kuboresha maadili katika taaluma ya uuguzi na ukunga.

Muuguzi Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Charles Kadugushi akitoa salamu kwa washiriki hao

Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wakuu wa Wilaya mara baada ya ufunguzi

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wasajili wa mabaraza ya kitaaluma yaliyopo chini ya wizara ya afya

Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Ziana Sellah akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Agnes Mtawa akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi hicho kinachofanyika jijini Dodoma.
 
……………………………………………………………………………
 
Na.Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma 

Wauguzi na Wakunga nchini wametakiwa kusimamia na kutoa huduma kwa kuzingatia miongozo iliyopo na kwa kutumia utaalamu wao ili kufikia malengo na matumaini ya wateja kwa weledi mkubwa kwa ajili ya ustawi wa Taifa. 

Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Idara Kuu Afya Edward Mbanga wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji kazi wauguzi wakuu wa wilaya kinachofanyika jijini hapa. 

Bw. Mbanga amesema kuwa wauguzi na wakunga ndio watendaji wakuu katika vituo vya afya kwenye ngazi ya jamii hadi Taifa hivyo kuwajibika na utawala bora utaboresha utendaji pia kuhakikisha kufikia malengo mbalimbali waliyojiwekea katika ngazi zote. 

“Viongozi mnatakiwa kuwa wabunifu, wachapa kazi, wenye nidhamu na mfano bora wa kuigwa katika utekelezaji wa majukumu yenu,kwahiyo ni lazima msimamie utoaji wa huduma uliyo mzuri na wenye heshima na utu.”Alisema .

Aidha, Kaimu Katibu Mkuu huyo aliwakumbusha washiriki hao kuwa katika huduma za uuguzi na ukunga ni ubinadamu zaidi na kuvaa viatu vya wagonjwa wao “hakuna aliyegongwa muhuri wa kuugua au kuwa mgonjwa akalazwa ,sisi sote ni wagonjwa watarajiwa kwahiyo kama ambavyo sisi tungependa kuuguzwa vizuri,kijibiwa kwa kauli nzuri basi tuhakikishe tunasimamia maadaili ya kazi”.Alisisitiza Mbanga. 

Hatahivyo alisema Serikali inawahakikishia itaendelea kufanya kazi pamoja na waauguzi kwa kutoa miongozo thabiti na kuhakikisha upatikanaji wa nyenzo muhimu katika hospitali na vituo vya kutolea huduma ya afya na kuboresha mazingira ya kazi yaliyo bora na salama. 

Kwa upande wa malalamiko Kaimu Katibu Mkuu alisema hivi karibuni kumekuwa na malalamko mbalimbali ya kiutendaji na kitaaluma kutoka kwa wateja wanaofika kupata huduma za kiafya na hivyo kuleta taswira mbaya kwa taaluma yao na kuonyesha hakuna usimamizi mzuri wa utoaji huduma za uuguzi na ukunga“tungependa wateja wetu watoe sifa badala ya malalamiko hivyo kikao hiki mje na mipango ya kuondokana na malalamiko kwani taaluma yenu ni zaidi taaluma. 

Kuhusu suala ya rushwa viongozi hao wamekumbushwa kuwa mstari wa mbele kupambana na rushwa na kuhakikisha inatokomezwa katika maeneo yao ya kazi kwani rushwa imekuwa ikilalamikiwa na kuripotiwa katika kada ya afya nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...