Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki, akisikiliza maelezo ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, kuhusu mifumo ya fedha, sekta ndogo ya fedha na madeni, pensheni na bajeti, alipotembelea katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki, (kulia) akisoma chapisho la Bajeti ya Wananchi alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto), akitoa maelekezo kwa watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi zake, alipotembelea katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, wa pili kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga na wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Bw. Mcharo Mrutu (kulia) akielezea mchakato wa Zabuni za Umma wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, katikati ni Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga. Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano wa Taasisi ya UTT- AMIS, Bi. Martha Mashiku, akifafanua jambo kuhusu masuala ya uwekezaji wa masoko ya fedha, mitaji na dhamana za Serikali, wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki (kulia) akizungumza jambo na watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki (katikati), Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki, akizungumza jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
(Picha na Peter Haule, WFM)
*******************************
Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Simiyu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki amehimiza kutumia lugha rahisi na mitandao ya kijamii kufikisha taarifa za masuala ya uchumi na fedha kwa wananchi.
Rai hiyo ameitoa alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Mhe. Kairuki alisema kuwa ni vema Kampuni za simu za mikononi, tovuti na mitandao mingine ya kijamii ikatumika kupeleka toleo la Bajeti ya Wananchi kulingana na mahitaji husika ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Pia ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kusimamia taasisi za umma kuhakikisha zinatoa fursa kwa makundi maalum kushiriki katika zabuni za umma kama ambavyo sheria ya ununuzi wa umma inavyoeleza.
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana wametakiwa kuongeza kampuni zilizo jiorodhesha kwenye Soko la Hisa kutoka kampuni 27 ili idadi hiyo ilingane na idadi ya kampuni zilizosajiliwa kwenye Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni-BRELA, zinazofikia zaidi ya elfu nane ili sekta ya masoko ya mitaji na dhamana yawe chachu ya kukuza uchumi wa nchi.
Ameipongeza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kazi nzuri ya kuandaa mipango ya kitaifa na usimamizi wa Sera za Bajeti na Fedha na kuwataka wataalam wa Wizara hiyo kuongeza juhudi zaidi ili kuiwezesha nchi kufanikisha malengo yake ya kuwahudumia wananchi wake.
Akimwongoza kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi, mkoani Simiyu, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo, Bw. Benny Mwaipaja, alimweleza Waziri Mheshimiwa Angellah Kairuki, kwamba Wizara ya Fedha na Mipango inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika kukuza pato la Taifa.
Aidha alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, imefuta kodi zenye kero zipatazo 105 katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuongeza tija kwa wakulima na kuwawezesha kuzalisha mazao kwa wingi.
Aidha alisema kupitia taasisi zake za Wizara imetoa mchango mkubwa katika kukuza masuala ya ushirika na mikopo kwa wananchi ambapo amesema Taasisi yake ya Self Microfinance pekee, imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 36.3 kwa vikundi vya wajasiliamali nchini kote.
Bw. Mwaipaja alibainisha kuwa taasisi za elimu ya juu zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango kikiwemo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) zimetoa mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa tafiti zinazofanywa na vyuo hivyo zinakidhi mahitaji ya kuisaidia jamii hususani katika kuandaa maandiko ya miradi pamoja na huduma za ushauri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mheshimiwa Angellah Kairuki, alikuwa amemwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa, kwenye siku ya Ushirika, wakati wa Maonesho ya siku ya Wakulima Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...