Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki, akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mohamed Kizuri kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na TTCL alipotembelea Banda la Shirika hilo wakati wa maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Puyo Nzalayaimisi (mwenye T-shirt nyeupe) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki, alipotembelea Banda banda la TTCL kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri M Kuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki amelitaka Shirika la Mawasiliani Tanzania TTCL, kuongeza nguvu kwa Kampuni yake Tanzu ya T-Pesa ili iweze kwenda na kasi ya ushindani wa Kampuni za kifedha hapa nchini.

Waziri Kairuki alitoa rai hiyo alipotembelea banda la TTCL katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Amesema kwa Sasa Shirika kwa linafanya vizuri ikilinganishwa na awali na kuongeza kuwa ili kuendelea kuliteka soko TTCL hawana budi kuwekeza katika Kampuni ya T-Pesa ili kuwawezesha wananchi na hasa Wakulima, Wavuvi na wafugaji kujiepusha kuporwa pesa zao baada ya mauzo kwakuwa fedha zao zitakuwa salama katika simu zao.

Waziri Kairuki alitembelea banda la TTCL akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kwenye Siku ya Ushirika iliyofanyika mkoani Simiyu katika msimu huu wa maonesho ya Nanenane.

Kauli mbiu ya Mwaka huu ya Maonesho hayo yanayofanyika katika Mkoa wa Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo ni "Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi chagua Viongozi Bora 2020"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...