Na Mwandishi Wetu, MOHA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kesho Agosti 16, 2020, anatarajia kuanza ziara yake ya kutembelea makambi na makazi ya wakimbizi katika Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii, jijini Dar es Salaam, leo, Waziri Simbachawene amesema, lengo la ziara hiyo ni kutembelea makambi na makazi ya wakimbizi hayo pamoja na kuwahamasisha kurekea nchini kwao kwa hiari.

Waziri Simbachawene pia amesema kwa takwimu ya Agosti 5, 2020, Wakimbizi waliopo nchini ni 289,664 , na Wakimbizi waliorejea nchini kwao ni 88,929, na idadi wanaosubiria kurejeshwa kwao kwa hiari ni Wakimbizi 2,972 na idadi wanaojiandikisha inaendelea kuongezeka kwa kasi.

"Kesho Jumapili Agosti 16, 2020, nitawasili mjini Kigoma asubuhi, na nitakutana na Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya mazungumzo, na baada ya hapo nitaanza ziara yangu kwa kutembelea Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma, alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, baada ya NMC ataelekea Wilayani Kasulu Mkoani humo ambapo atatembelea Kituo cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), na kuzungumza na Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya Kambi hiyo," alisema Simbachawene.

Pia Waziri Simbachawene alisema Agosti 17, 2020 atatembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo na Kambi ya Mtendeli iliyopo Wilaya ya Kakonko Mkoa huo wa Kigoma, na pia atazungumza na wakimbizi katika kambi hizo kupitia mikutano ya hadhara.

"Baada ya kutembelea kambi tatu za Wakimbizi za Mkoa huo wa Kigoma, tarehe 19 nitafanya ziara katika Mkoa wa Katavi na nitaonana na Mkuu wa Mkoa huo kabla ya kuelekea Makazi ya Wakimbizi ya Mishamo Wilaya ya Tanganyika na Katumba iliyopo Wilayani Tanganyika Mkoani humo," alisema Simbachawene.

Waziri huyo anatarajia kumaliza ziara yake Agosti 20, 2020, katika Mkoa wa Tabora baada ya kutembelea Makazi ya Wakimbizi ya Ulyankulu Mkoani humo na kuzungumza na wakazi wa Makazi hayo.

Katika ziara hiyo ya siku tano, Waziri Simbachawene ataambatana na Viongozi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi na Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kigoma, ambapo pia watafanya kikao na viongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Nchini. 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...