Na Amiri Kilagalila,Njombe
Taasi binafsi na za Umma wilayani Njombe zimetakiwa kuketi katika meza ya majadiliano katika masuala ya kibiashara na kiuchumi badala ya kila sekta kufanya mambo yake.

Katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa baraza la biashara wilaya ya Njombe mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amesema kuwa mkutano huo ni muhimu na kiungo kikubwa cha uchumi kwa wananchi kwa kufanya majadiliano ya pamoja juu ya changamoto zilizopo.

“Tuna mambo mengi sana Njombe ambayo tunaweza kuyafanya lakini sekta binafsi iko peke yake na sekta ya umma iko peke yake,watu wa Njombe ni hodari wa kufanya kazi sasa tumekutana ili tubadilike na tuwe wa moja kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika wilaya yetu”alisema Ruth Msafiri

Mgeni wa heshima katika ufunguzi wa mkutano wa baraza hilo ni katibu mtendaji wa baraza la biashara taifa Dokta,Godwin Wanga ambaye amesema hakuna uchumi imara pasina mashirikiano baina ya sekta binafsi na umma na katika kufanikisha hilo lazima kuwepo kwa  majadiliano.

“Mnaweza msijatambue lakini watu wa Njombe mnatoa mchango mkubwa sana katika taifa letu kupitia kilimo na mna mazao ambayo yanatusaidia sana hata kuingiza fedha za kigeni,mfano Mbao”alisema Dkt,Godwin Wanga

Awali katibu mtendaji wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA mkoa wa Njombe bwana Leo Tamambele amesema kuwa vikao vya baraza la biashara husaidia sana kukuza uchumi ndani ya wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla.

“Kwa kweli tunajiskia amani sana na tunaahidi kufanya kazi kwa bidii kupitia baraza hili”  alisema Leo Tamambele
  DKT,Godwin Wanga, katibu mtendaji wa baraza la biashara Taifa akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyabiashara wilaya ya Njombe katika zoezi la ufunguzi wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa wilaya ya Njombe.
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyabiashara kutoka sekta binafsi na taasisi za kiserikali wakiwa makini kusikiliza umuhimu na majukumu ya baraza hilo wakati wa ufunguzi wa baraza lililofanyika wilayani Njombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...