Na Pius Ntiga-Siha.


Zaidi ya ajira 2,000 zimepatikana katika Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro kwa kipindi cha miaka mitano za wananchi kufanya kazi katika miradi mbalimbali ukiwemo wa Shamba la Mwekezaji la Maparachichi-Africado.


Miradi hiyo mikubwa ya Mwekezaji Africado lililopo Kijiji cha Kifufu pamoja na ule wa Shamba la uzalishaji wa Mayai ya Kisasa lenye ukubwa wa hekari 507 lililopo Kijiji cha Namwai, la Mwekezaji Irvine Family, imezalisha ajira zaidi ya 700 Kati ya 2,000 za wananchi kuanzia mwaka 2015-2020.


Akizungumza na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM ikilenga kuainisha mafanikio ya serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, 

Meneja Utawala wa Shamba la Africado, Berinda Meena, amesema Shamba hilo limesaidia kupatikana kwa ajira 500 za wananchi wa Siha ambazo zimefanikisha kujikwamua kiuchumi na kujiongezea kipato.


Chini ya Mafanikio shamba hilo la Africado lenye uwekezaji wa Mabilioni ya Shilingi limekuwa likisaidia pia wafanyakazi kujengewa uwezo wa ujuzi wa kilimo kwa kufunga Vikonyo,  ambapo sehemu kubwa ya wafanyakazi Wana mashamba yao binasfi.

Amesema wanyakazi hao wamekuwa wakipatiwa pembejeo bure na Mwekezaji huyo ambapo mazao yao huyauza pia katika Shamba ya huyo Mwekezaji Africado ambapo Mwekezaji wake ni James Pasoz raia wa Ujerumani.


"Tangu Mwekezaji huyu awekeze katika shamba hilo ambapo Sasa yapata miaka 10 wamekuwa wakizalisha maparachichi na kuyauza ulaya na Uarabuni" amesema Berinda.


Kwa mwaka huu zaidi ya Tani 3,600 amesema zimezalishwa katika shamba hilo na kuuza nje ya nchi.

 

"Maandalizi ya shamba la Maparachichi ni miaka mitatu kuanzia hatua ya kupanda Miche hadi kuvuna kwa kutumia mbegu ya Hasi inayokuwa haraka" alisema.


Aidha, amesema Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kwa kutoa leseni kupitia EPZ na msamaha wa kodi na kuwezesha eneo kubwa kwa kuweka mtaji mkubwa, na hivyo ameipongeza Serikali kwa kumsaehe pia VAT kwa vitu anavyonunua kwa ajili ya shamba hilo.


Pia Berinda amesema Mwekezaji huyo amekuwa na mahusiano mazuri kati yake na serikali.


Aidha, amesema Mazingira ya uwekezaji sasa ni mazuri kwa kiasi kikubwa wamekuwa na mazingira ambayo yamesaidia kampuni hiyo kukuwa kwa kiasi kikubwa.


pia amesisitiza kuwa bado wanatafutwa maeneo mengine ya kuwekeza zaidi wilayani Siha.


"Shamba hilo limekuwa na msaada mkubwa kwani kipato kinachopatikana  kimekuwa kikisaidia kukuza uchumi wao pamoja na kujenga shule ya msingi Karagoha na kutoa kampeni ya matibabu bure ya Macho" amesema.


Wakati huo huo, Meneja Mwendeshaji wa Shamba la Mayai ya Kisasa la Joseph Kasegama, amesema Shamba hilo limepunguzaa upungufu uliokuwepo nchini wa upatikanaji wa vifaranga vya Kuku na limesaidia ajira 120 za wananchi wa Siha na kuongeza pia Mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha.


"Shamba hilo la Irvine Family lenye hekari 507 lina Mabanda 507 yenye uwezo wa kuchukua Kuku 9,000" Alisema.


Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu, ameipongeza serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli kwa kupeleka kiasi kikubwa cha fedha za maendeleo katika Wilaya hiyo ambazo pia zimewezesha kukarabati pia Hospitali ya Wilaya ya Siha.


Chini ya fedha hizo Hospitali ya Kibong'oto inayotibu pia watu wa Kifua Kikuu-TB, imepelekewa shilingi Bilioni-7 huku Hospitali ya Wilaya ya Siha imepokea shilingi Bilioni-2 zilizofanya ukarabati Mkubwa.


Aidha, amesema zaidi ya bilioni 50 zimetumika kujenga barabara za lami wilayani humo sanjari na kurahisisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na Salama.


Pia amesema Mpango wa elimu bure umesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya Msingi na sekondari wakiwemo wa jamii ya Kimasai.


"Ni kwamba Ukanda wa Kasikazini haujasaulika, kwani kumekuwa na maneno kuwa Ukanda huu umesahaurika kitu ambacho sio kweli" Alisema Buswelu.


Mkuu huyo wa Wilaya ya Siha, ambaye Katibu Tawala wake wa Wilaya hiyo ni Joseph Mabiti, DC  Buswelu, amesema hodpitali hiyo yenye ukubwa wa Hekari 20 ikimalizika itakuwa na uwezo wa kutibu wagonjwa hata kutoka Longido pamoja na Arumeru.


Aidha kuhusu suala la wakulima na wafugaji amesema sasa hali iliyopo wilayani hiyo hakuna magomvi kwenye zaidi ya hekari 700 zimetengwa kwa ajili ya wafugaji.


Kuhusu mahusiano na wawekezaji amesema Ni mazuri na hivyo kuwataka watu kupuuza kauli zinazotolewa kuwa hakuna mahusiano mazuri ya wawekezaji na serikali.


Akizungumzia Kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea, Buswelu,  amewataka wanasiasa kunadi Sera zao kwa utulivu na waache mihemuko na aakawataka wananchi kutekeleza haki yao ya msingi kwa kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 mwaka huu wakachague viongozi watakaowaletea  maendeleo ya haraka.


Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Siha, Dkt Andrew Method, amesema hivi karibuni mashine ya X-ray itafungwa na hivyo kupunguza changamoto ya wanachi kwenda kutafuta huduma ya vipimo KCMC pamoja na Hospitali ya Mawenzi ya Mjini Moshi.


Aidha Hospitali hiyo ndani ya wiki chache zijazo majengo ya Huduma na mama na mtoto yataanza kutumika, ambapo katika Hospitali hiyo vifo vinavyotokana na uzazi vimepungua na kifo kimoja kwa mwaka.


Aidha, Dkt Method amesema hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kuwa na jengo la kisasa la kuhifadhi miili 20 ya marehemu kwa wakati mmoja.


Pia amesema ndani ya miezi mitatu ijayo Hospitali hiyo ya Siha itapokea kiasi kikubwa cha dawa ambacho kitatoshereza Hospitali hiyo na hata kuzidawa katika vituo vingine vya Afya nje ya Wilaya hiyo.


Nao wananchi pamoja na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha, wamepongeza uboreshaji wa Hospitali hiyo ambayo inatoa huduma kubwa za kibingwa ambazo walikuwa wakizipata nje ya Wilaya hiyo ya Siha.

 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...