Charles James, Michuzi TV

WANANCHI wa Mkoa wa Dodoma wameaswa kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 mwaka huu kumpigia kura nyingi za ndio mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Dk John Magufuli kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwenye mkoa huo kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.

Hayo yamesemwa na Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile alipokua kwenye ziara ya vikao vya ndani Wilayani Kongwa alipoenda kumuombea kura Dk John Magufuli na madiwani wa Kata za Jimbo hilo.

Kongwa ndio jimbo la Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye tayari ameshapita bila kupingwa hivyo Ditopile amewaomba wananchi wa Kongwa kumpa heshima Magufuli ya kumchagua kwa kishindo.

" Dodoma tuna kazi kubwa sana ya kuhakikisha tunaongoza kwa kura za Rais, kwa miaka mitano ya kwanza ya Magufuli ni wazi Sisi ni Mkoa tulionufaika nae kwa kiasi kikubwa, amefanya mambo ambayo hayajawahi kufanyika kwa miaka yote.

Kwanza amehamishia Makao Makuu hapa Dodoma pamoja na serikali yote na yeye akiwepo, hapa Kongwa yenyewe mmejengewa vituo vitatu vya afya na sasa kuna Chuo cha Ufundi kikubwa Kabisa cha Veta kinajengwa na kiko tayari kukamilika, mnataka tupewe nini zaidi Ndugu zangu?," Amesema Ditopile.

Amewaomba wanawake wa Umoja wa Wanawake wa CCM Wilaya ya Kongwa kuongoza mapambano ya kutafuta kura za Rais na madiwani na kuhakikisha wagombea wao wote wanaibuka na ushindi mkubwa ili waweze kushirikiana kusongesha maendeleo.

Amewataka wana-CCM kuepuka makundi na misuguano katika kipindi hiki cha kampeni badala yake wajikite kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura huku wakieleza mambo yote mazuri ambayo yamefanywa na serikali kwa kipindi cha miaka mitano.

Akiwa ziarani Kongwa, Ditopile pia ameshiriki msiba wa mwanachama mkongwe wa CCM katika eneo la Sabasaba, Mzee Yona Lengwale aliyefariki akiwa na miaka 100.

" Kwa niaba ya Chama chetu na Mbunge wa Jimbo, Spika Ndugai nimekuja hapa kuungana na nyinyi na kutoa rambirambi zetu, tunauheshimu mchango wa Mzee wetu Yona kwa Nchi yetu na chama pia, niwahakikishie kuwa tutaendelea kuyaenzi mazuri yake lakini pia kuwa na familia yake katika kipindi hiki kigumu.
 Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Mariam Ditopile akizungumza na Wanawake wa UWT Wilaya ya Kongwa alipofika kumuombea kura mgombea Urais wa chama hicho, Dk John Magufuli na madiwani wote.
 Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Mariam Ditopile akizungumza na waombolezaji katika msiba wa Mzee Yona Lengwale ambaye ni mwanachama wa chama hicho.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile akizungumza na wakina mama wa UWT Wilaya ya Kongwa katika kikao cha ndani ambapo pamoja na kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli lakini pia amewaeleza mafanikio ambayo yamepigwa na serikali ya awamu ya tano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...