Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kigoma

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amesema kwamba walipoingia madarakani mwaka 2015 walifufua zao la Mchikichi kwa lengo la kuufanya Mkoa wa Kigoma kuwa juu kiuchumi.

Dk.Magufuli amesema hayo leo mbele ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma ambapo amesema katika kuhakikisha zao hilo linafufuliwa aliwahi kumtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kama hatua ya kufufua zao la mchikichi.

Amesema amesikia watu wakisema wamefufua zao hilo"Nikimtuma mtu mwingine anasema yeye, mimi nilimtuma Majaliwa kwa lengo la kufufua zao hili,Kigoma nawapend sana, nataka Kigoma ipande juu."

Hata hivyo amesema kwamba alipoingia madarakani alisema hawezi kuucha Mkoa wa Kigoma kuwa nyuma kimaendeleo, hivyo alitengeneza mkakati wa kutosha kwa kuteua mawaziri watatu kutoka Mkoa huo.

Amesema lengo la kuteua mawaziri hao ni kuifanya Kigoma kuwa katika ramani ya nchi na mawaziri hao aliwapa wizara nyeti.

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...