Zaidi ya wachimbaji wadogo 100 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Geita wamepata mwanga mpya uliojaa matumaini juu ya mbinu mbalimbali za utafutaji , uchimbaji na Uchenjuaji wa Madini kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

GST kupitia wataalam wake wametoa mwanga mpya  kwa wachimbaji wadogo kupitia uwasilishaji wa mada juu ya matumizi ya mbinu za kisasa za utafuta  madini.

GST kupitia wataalam wake imetoa mada husika katika njia mbalimbali ikiwemo namna Bora ya Utafutaji , Uchimbaji  na Uchenjuaji wa Madini.
Sambamba na semina hii GST ilipata fursa ya kutembelewa na wachimba wadogo wakiwa na hamu ya kuona vifaa vya Utafiti wa madini pamoja na kufahamu jinsi taarifa za Jiolojia zinavyochakatwa.

Akiongea na GST mapema baada ya semina kuisha mchimbaji mdogo ambaye pia ni mwanachama Cha wachimbaji wadogo mkoani Geita GEREMA Mariam Kome aliishukuru GST kwa kutoa mwanga mpya hususani katika Uchenjuaji wa Madini.

Naye mchimbaji mdogo kutoka Mwanza James alisema semina  hii italeta tija katika Utafutaji wake , uchimbaji kwani kwa mara nyingi amekuwa akichimba bila kujua namna za uchimbaji Ila kupitia semina hii nimepata mwanga.

Semina hii ya siku tatu imeisha Leo huku wachimbaji wakiendelea kupata Elimu kupitia maonesho ya vitu mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...