Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari.
Meneja wa Tawi la Dar es Salaam wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Sekunda Titus akizungumza wakati wa kumkaribisha mkuu wa Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Chuo hicho kilivyojipanga katika utoaji wa elimu bora yenye utaalam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA) kimesema kuwa kimeongeza kozi 17 kutokana na mahitaji kuongeza katika utoaji wa huduma utaalam kwa wananchi pamoja kupanua uwigo wa soko la ajira

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka amesema kuwa kwa Tawi la Dar es Salaam wamehama jengo katika barabara ya Pugu na Kuhamia katika Jengo la TTCL Kijitonyama ikiwa ni kusogeza huduma kwa wanafunzi kwa urahisi wa kufikika.

Amesema katika kozi zilizoongezeka ni pamoja ni lugha kwa Kichana kutokana na kuwepo kwa wachina wengi wanaofanya miradi mbalimbali pamoja na watalii ili waweze kuwasiliana nao.

Amesema kati ya kozi ni pamoja ni kozi ya ujasiriamali kwani wengi wanafanya biashara lakini hawana utaalam hivyo kozi  itawajenga kuinuka kiuchumi kwa kupangilia biashara zao.

Profesa Sedoyeka amesema kuwa wanakozi za shahada ya pili ambazo shahada ya Bima, Bank ambazo  zitakafanya wawe wana utaalam zaidi katika utoaji wa huduma kwa jamii.

Aidha amesema pamoja na kuanzisha hizo kozi wameangalia upande wa waandishi na kuweka kozi  ya Multimedia ambapo katika eneo la mitandao ya kijamii wataweza kumudu zaidi kuliko ilivyo sasa.
Profesa Sedoyeka amesema Chuo licha ya kutoa elimu pia wanawajenga wanachuo kimaadili ili elimu wanayaoipata iweze kuleta matokeo chanya katika taifa.

Hata hivyo Profesa Sedoyeka aliongeza kuwa kozi zote zilizoongezeka ni kutokana na mahitaji ya soko huku kozi zingine zilizokuwepo zikiendelea kuboreshwa.

Amesema Chuo kimekuwa kinaongeza matawi yake katika kusogeza huduma kwa wananchi pamoja na kuwa vpindi vinavyoanza mchana ili wafanyakazi waweze kusoma kiurahisi.

Amesema katika kipindi cha Ugonjwa wa Virusi vya IAA ilifunga Chuo lakini walikuwa wanaendelea na vipndi kama kawaida kutokana mifumo ya mitandao hadi wanachuo wakashauri kuendea kusoma kwa mtandao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...