Charles James - Michuzi TV,Zanzibar


KAMPENI za Ubunge na Uwalilishi Jimbo la Chumbuni mkoa wa Mjini visiwani Zanzibar zimezinduliwa rasmi huku wananchi wakiombwa kukichagua Chama cha Mapinduzi CCM ili kiweze kuendelea na kazi iliyokwishaianza.


Mgombea wa Ubunge jimbo hilo, Ussi Salum Pondeza na mgombea kiti cha baraza la uwakilishi, Miraji Kwanza wakihutubia wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni hizo wameomba kura kwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi za kwao wenyewe na za madiwani wa chama hiko.


Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Ussi Salum Pondeza amesema kwa miaka mitano Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa visiwani Zanzibar ya kuinua uchumi, kuboresha sekta ya Afya, elimu na miundombinu hivyo kuomba wananchi wawachague tena ili wazidi kuleta maendeleo.


Amesema yeye binafsi mambo yote aliyoahidi katika uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2015 ameyatekeleza kwa kiasi kikubwa hasa yale ya kijamii na kama akichaguliwa kwa mara ya pili basi ahadi yake ni kukuza uchumi wa wananchi wake kupitia vijana.


" Mengi mliyonituma kuyafanya mwaka 2015 nimeyatekeleza kwa kiwango kikubwa sana, mathalani kwenye Afya tulikua hatuna gari la wagonjwa ila leo tuna Ambulance nzuri na ya kisasa kuliko sehemu yoyote Zanzibar, ina vifaa vyote hadi vya upasuaji.


Ahadi yangu kwenu sasa ni kuwa na kituo kikubwa cha afya cha Chumbuni kuliko hiki tulichonacho ili kuepuka changamoto ya wananchi wetu kutembea umbali mrefu kwenda Mnazi mmoja, niwahakikishie mkinichagua mimi na wenzangu wa CCM tutafanikisha kituo hiko," Amesema Pondeza.


Kuhusu uchumi Pondeza amesema kama ilivyo kiu ya mgombea Urais Dk Mwinyi ya kuinua uchumi wa Zanzibar kuwa wa Bluu yeye nae ni muumini wa uchumi na hivyo atashirikiana na vijana wa Chumbuni kwa kuwainua kwenye vikundi vya uvuvi wa kisasa ambao anaamini utakua msaada katika kukuza uchumi wa Nchi hiyo na wananchi wa Jimbo lake.


Nae mgombea uwakilishi, Miraji Kwanza amewaomba wananchi kuachana na maneno ya wapinzani ambayo mengi wanayoyazungumza ni porojo zisizotekeleza zaidi ya kuongelea kuhusu uvunjifu wa amani na siyo maendeleo ya wananchi.


" Ukimsikiliza mgombea wetu Dk Mwinyi na wale wenzetu utagundua maendeleo ya Zanzibar yatapaa chini ya Mwinyi tu, wenzetu kila kukicha wanaongelea uvunjifu wa amani na machafuko, tuachane nao tuwaepuke na ili kuifanya Jimbo letu na Nchi yetu kung'ara basi Oktoba 28 twendeni tukachague wagombea wote wa CCM," Amesema Kwanza.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar (kulia) akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni kupitia Chama hicho, Ussi Salum Pondeza kwenye uzinduzi wa kampeni za Jimbo hilo.

 Mgombea Ubunge Jimbo la Chumbuni, Zanzibar kupitia CCM, Ussi Salum Pondeza akinadi Sera zake na Ilani ya Uchaguzi ya Chama chake katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni zake kwenye Jimbo hilo.

 Mgombea Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Chumbuni visiwani Zanzibar, Miraji Kwanza akihutubia wananachi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za jimbo la Chumbuni.

 Wananchi na viongozi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la Chumbuni wakifuatilia burudani ya vikundi vya ngoma za asili za Zanzibar.

 Mgombea Ubunge Jimbo la Chumbuni CCM, Ussi Salum Pondeza akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni zake. 

Wananchi mbalimbali wa Jimbo la Chumbuni visiwani Zanzibar waliojitokeza kuwasikiliza wagombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Ussi Salum Pondeza na mgombea kiti cha baraza la wawakilishi, Miraji Kwanza kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...