*Polepole asema kuna Chama cha upinzani kinahusika, ushahidi wote wanao
*Wasema waliohusika wachukuliwe hatua haraka, umma utajua ukweli 


Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Dodoma.

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimemwomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini(IGP), Simon Sirro kusimamia uchunguzi/upelepezi wa kifo cha Mwenyekiti wa UVCCM Emmanuel Mlelwa kwani kuna chama kimoja cha upinzani kimehusika kufanya mauji hayo.

Ombi hilo, limetolewa leo Septemba 27,mwaka 2020 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humprey Poleple wakati akitole ufafanuzi baadhi ya mambo ya upotoshaji ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya wagombea wa upinzani kwenye kampeni zao.

Polepole amesema kuwa Septemba 21 mwaka huu, kijana wa CCM Mlelwa ambaye ni mwenyekiti wa UVCC, Seneti Mkoa wa Iringa ambaye kwao ni Njombe akiwa kwenye mapumziko yake ya Chuo Kikuu amekwenda kule kushiriki katika kampeni alikamatwa na kutekwa lakini baadae alikutwa akiwa amefariki.

"Hayati Mlelwa alikuwa ni kijana msomi amepikwa, kule amepiga kampeni vizuri, pale chama cha Mbowe wamemuelewa madiwani walimuelewa. Ushahidi jeshi la Polisi tafadhali wakati mwingine upelelezi unachukua muda bila sababu za msingi , zipo taarifa chama cha upinzani kuhusika.
"Na tunataka jeshi la polisi, ukweli unafahamika, watu viongozi wa chama cha upinzani.Sitaki kusema wamefanya mawasiliano na huyu kijana, wamemteka wamepotea nate, Kibena Bwawani ndiko ambako mwili wake umekutwa, amepigwa ameumizwa,"amesema.
Amefafanua kuwa ushahidi upo na wamekamatwa watu hivyo Sirro alimamie ili upelelezi ukamilike na hatua kali za mfano zichukuliwe kwakuwa haiwezekani kuwepo chama mbinu zao mauaji wala cha kuteka watu.

"Kiongozi huyo alikuwa na ndoto zake, alikuwa anasoma chuo kikuu, lakini ndoto zake zimakatwa, hao hao viongozi ndio wamehusika, wamepatikana, tunafuatilia kwa karibu sana, ni maisha gani haya,"amesema.

Amefafanua kuwa pia kumekuwepo na matukio ya kutengeneza na kwamba ushahidi upo, mfano ofisi kuchomwa huku akilitaka Jeshi la Polisi kufanya upelelezi wa haraka ili watanzania wajue ukweli.

Amesema kwa kawaida shetani sifa zake tatu ambazo ni uongo, kuua na kuharibu huku akieleza moja ofisi zao wanachoma moto, piki ushahidi upo, lakini tatu kuua na kwamba polisi wasicheleweshe ukweli kwakuwa hawajaanza leo kutoa kauli za kuchonganisha watu.

Ameweka wazi kuwa hata ukienda Zanzibar mchezo ni ule ule ambapo mara kwa mara Maalim Seif Sharrif Hamadi Mgombea wa ACT-Wazalendo amekuwa akiwaambia watu wachukue mapanga, wachukue mundu na siku chache baadae watu wakapigwa mapanga.

"Tunaipeleka wapi hii nchi?...Tunalitaka Jeshi la Polisi hatua kali zichukuliwe iwe mfano, watanzania wajue aina ya wapinzani ambao tunao katika nchi hii, wamekuwa na kauli za kuhamasisha vurugu,tumeamua kukaa kimya.

"Pale Songwe wako madiwani wametoka chama cha Mbowe wamehamia ccm, mashamba yao yamekatwa maheka kwa maheka. Pale Momba kuna diwani amepigwa risasi karibu 30, hatuzungumzii haya mambo kama mtaji wa kisiasa, watu wanaendelea kukamatwa, tuna ushahidi, sisi sio kama chama chao mtu akiumizwa wanazunguka naye kama mtaji wa kisiasa. polisi chukueni hatua,"ameeleza.

Hata hivyo amesema kuwa Lissu amekuwa mtu wa kwanza kuhamasisha vurugu na atashangaa kama mahakama ya kimataifa watakaa kimya kwakuwa yeye anasubiri na kama haitachukua hatua yeye atasubiri hilo.

"Lugha yao ukiisikia utabaini ni ya mawakala, wanataka watu waingie mtaani, watu hawajasahau ya Libya, duniani hakuna siri kwenye mambo ya siri, watoto wake wanao uraia wa nchi nyingine, mwenyewe ana uraia wa nchi nyingine, tunafahamu.

"Unajua tangu ameenda kutibiwa nje, sijui nini kimeotokea, kila kitu anafikiria nje, aende akagombee huko, unaposikia mtu kibaraka ndio huyu, kauli zile sio za zake, kuna wazungu kadhaa wanaongea lugha kama yake, wakati wa corona, wakati wanapigwa risasi hakuna aliyetoa kauli hata moja, leo hi wanasema sisi sio kitu,"amefafanua.

Amesisitiza kuwa hata ilani yao ipo mpeche mpeche, mlenda mlenda, wanataka kuuza nchi yetu tumewashutukia na watahakikisha wanabana kila ili maendeleo yazidi kufanyika nchini.

Ameongeza kuwa Lissu amekuwa akituhumu viongozi kwenye mambo kadhaa ikiwemo katika ardhi na kuwataka watu wa maeneo husika wawe mstari wa mbele kusema ukweli badala ya kuacha upotoshaji ukiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...