Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome



Na Vero Ignatus,Arusha


Wizara ya Katiba na Sheria imeendesha Kikao cha Makatibu wakuu na wakuu wa Taasisi za Serikali kujadili mfumo jumuishi wa uangalizi wa utajiri wa Asili na Rasilimali za nchi na kuwaleta wadau pamoja na kuangalia sheria za mamlaka ya nchi kuhusu umiliki wa utajiri na maliasili za nchi 21 SEP 2020


Akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome,katika kikao hicho kilichofanyika,Katika Ukumbi wa Hotel ya Mountmeru,alisema Tanzania,inaweza kuendelea kwa kutumia utajiri na maliasili ilizonazo hususan katika kipindi hiki ambacho tayari imeingia katika uchumi wa kati ikiwa na maana imeelimika na inaendelea kuelimika,pia upo uongozi unaothubutu na Kuna uelewa mkubwa 


Aidha Prof.alisema kumekuwa na ongezeko la kiwango cha faida na kipato katika uwekezaji Sekta ya madini ambapo inakua kwa zaidi ya 17.7% ,inachangia kusafirisha bidhaa nje ya nchi kwa 51.9% na mapato ya Bilioni 168 kwa mwaka 2015 hadi 528 kwa mwaka 2020,ambapo fedha zilizokuwa zikipotea kwenye utajiri wa maliasili zimeanza kuokolewa na kupelekwa kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya watu


Alisema kuwa kila kipande cha Tanzania ukitembea na kufanya utafiti utagundua kuwa kuna kitu fulani cha asili kipo na kinastahili kuwa sehemu ya utajiri ,au rasilimali,japokuwa vipo vingiambavyo wajanja wameshavichumua,(Nje na ndani ya nchi) na wamevifanya Mali yao


"Nchini Ujerumani Kuna Dinassour kutoka Tendaguru ambaye anaiingizia nchi hiyo mapato ya Aina mbalimbali kutokana na ama maonyesho ,utalii au utafiti,lakini Kuna taarifa mbalimbali zilizoo huko kuhusu utajiri na rasilimali zetu ambazo pia taarifa hizo huuzwa kwa watu mbalimbali hususani watafiti na wawekezaji".alisema Prof.


Pro.Mchome alisema Sheria iliweka mwongozo na makatazo na kuwathibitishia Watanzania kuwa utajiri na maliasili iliyopo ni Mali yao na wazitumie kwa faida yao,pia inabainisha kuwa siyo sawa kuingia katika mahusiano yeyote ya Kimataifa ama vinginevyo iwapo mahusiano hayo hayana manufaa kwa wananchi wa Tanzania na iwapo mahusiano hayo Ni kinyume na matarajio ya Sheria.


Aidha alisema changamoto bado zipo ambapo zipo baadhi ya sheria haziongei vizuri,mifuko ipo mingi,inahitaji utaratibu wa kuhuishwa ili kuleta tija zaidi, hivyo wanayo kazi ya kukamata uwigo wote unaohusu utajiri na maliasili ambapo msukumo upo kwenye madini ,gesi,na mafuta ili kuinua fursa kwenye maeneo mengine ya utalii,maji,mimea,na anga.


Katika eneo la utatuzi wa migogoro ya ndani ya nchi Prof.Mchome alisema sheria inatambua nchi imekuwa huru miaka 59,mifumo mingi imeendelezwa na inatumika,

alisema kuwa migogoro siyo Jambo jipya liijitokeza itatuliwe hapahapa nchini na hiyo siyo kuokoa fedha tu bali linaeezesha mifumo kuendelea kukua,wataalam kupata ujuzi na maarifa,kukuza ajira.


Kwa upande wake Mwadhiri Mwandamizi wa uchumi Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt.Abel Kinyondo alisema kuwa ili Watanzania waweze kunufaika katika utajiri huo lazima waunganishwe katika mnyororo wa thamani pamoja na kuwepo kwa wazawa wanaonunua na kusambaza bidhaa mbalimbali


Aidha akisisitiza kuwa mikakati ya kiuchumi,kwa kutumia maliasili iliyopo kama malikale,uvuvi ,wanyamapori iwe kwa kila mtanzania anapewa fursa ya kushiriki katika uwekezaji, biashara inayohusu utajiri na maliasili za nchi kupitia njia mbalimbali ,ambapo serikali ina haki na wajibu kwa niaba ya wananchi,ya kuwa mbia au hisa katika eneo hilo la utajiri na maliasili,kwa uwekezaji wa mabenki ,masoko ya hisa na ushirika


Alisema utajiri asili ni pamoja na Ardhi,matabaka ya ardhi,Gesi asilia,mafuta,hewa,Maji,mabonde ya maji na vyanzo mbalimbali vya maji ,mimea ya asili Ikiwemo miti ya dawa za asili,wanyama pori au wanyama asili Ikiwemo maeneo walipohifadhiwa ,rasilimali asilia za kijenetiki katika mimea na wadudu ambao wanasifa za kijenetiki ambao wanalindwa kwaajili ya thamani yao kwa aajili ya vizazi vijavyo vya Sasa na baadae.


Mwisho





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...