Na mwandishi wetu, Michuzi TV

 CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeandaa mafunzo maalumu ya usimamizi wa madeni na marejesho  yenye mlengo wa kuwawezesha washiriki kuelewa zaidi kuhusiana na usimamizi huo kitaifa na kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chuo hicho, imeelezwa kuwa mafunzo hayo yatafanyika katika chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam kuanzia tarehe 2 hadi 4 Novemba  mwaka huu.

Aidha imeelezwa kuwa mafunzo hayo yamewalenga mameneja mikopo na Fedha, maafisa uhusiano na wakaguzi.

Imeelezwa kuwa mafunzo hayo  yatabeba mada mbalimbali ikiwa pamoja na; Usimamizi wa madeni na marejesho, sera za usimamizi wa mikopo,ufuatiliaji na tathimini za mikopo pamoja  na mikakati na mbinu za ukusanyaji madeni.

Vilevile imeelezwa kuwa kupitia mafunzo hayo washiriki watatunukiwa vyeti kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na vitawatambulisha katika masuala ya usimamizi wa madeni na marejesho kitaifa na kimataifa.

Washiriki wa mafunzo hayo wameelekezwa  kuwasiliana na Mratibu wa mafunzo hayo,  Dkt. Erick Lusekelo Mwambuli kupitia barua pepe; Erick.mwambuli@ifm.ac.tz au  0713 537913/0754 338767 ili kuweza kupata taratibu za kushiriki mafunzo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...