Naibu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Julieth Magandi akizungumza na baadhi ya wanachama wakati wa kuhitimisha mafunzo yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili katika Hospitali ya Mloganzila. 

Baadhi ya wanachama walioshiriki mafunzo hayo wakimsikiliza mada. Afisa Ushirika Manispaa ya Ubungo Bw.Omari Mkamba wakati akitoa elimu kwa wanakamati juu ya umuhimu na faida za kujiunga na SACCOS. 

************************************* 

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendesha mafunzo ya uanzishwaji wa kamati ya SACCOS kwa watumishi yenye lengo la kuwawezesha watumishi kupata mikopo yenye riba nafuu. 

Afisa Ushirika Manispaa ya Ubungo Bw. Omari Mkamba ameeleza kuwa lengo la SACCOS ni kuwawezesha wanachama kujiwekea akiba kwa kununua hisa na kupata mikopo yenye riba nafuu itakayoweza kukidhi mahitaji. 

“Lengo la SACCOS ni kuwawezesha wanachama kupata mikopo kwa riba nafuu ambapo mwanachama atanufaika na aina mbalimbali ya mkopo ikiwemo mkopo wa dharura,mkopo wa maendeleo, mkopo wa vikundi pamoja na mkopo wa elimu” amesema Bw. Mkamba. 

Bw. Mkamba ametaja faida mbalimbali ambazo mwanachama atanufaika nazo atakapoamua kujiunga na SACCOS ikiwa ni pamoja na mwanachama kujenga tabia ya kujiwekea akiba, kuchochea ukuaji wa uchumi na shughuli za kijamii, kupata mikopo yenye riba nafuu, kupata mikopo kutoka taasisi kubwa za kifedha pamoja na kujenga ushirikiano baina ya wanachama. 

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesisitiza kuwa ni jukumu la wanachama kuhakikisha wanachagua viongozi waadilifu na makini watakoweza kusimamia maslahi ya wanachama wote. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi,Rasilimali Watu na Utawala Bi. Njoikiki Mapunda amesema kuwa lengo la kuanzisha SACCOS ni kuwasaidia watumishi kukidhi mahitaji yao na kuepuka kutegemea mwajiri pekee. 

Mafunzo hayo yameenda sambamba na uchaguzi wa wajumbe sita wa kamati ya uanzishwaji wa SACCOS ya MNH-Mloganzila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...