MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduziu ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akihutubia Wananchi wa Wilaya ya Wete Pemba na kumuombea Kura Mgombea wa Urais wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Mwinyi na Rais wac Tanzania Mhe. John Magufuli na Wabunge, Wawakilishi na Madiwani mkutano uliofanyika Uwanja wa Mpira Gando.(Picha na Ikulu)
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Wilaya yac Wete Pemba na kuomba kura na kuwaombea Kura Wagombea Ubunge,Uwawakilishi na Udiwani Kisiwani Pemba, mkutano huo wa kampeni umefanyika katika uwanja wa mpira Gando Pemba.
MKE wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi akizungumza na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa mpira Gando Wilaya ya Wete Pemba.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Mwinyi, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa mpira Gando Wilaya ya Wete Pemba.
MWANACHAMA wa Chama cha ACT-Wazalendo Bi.Rahma Sheha Hamad akitangaza kukihama Chama cha ACT- Wazalendo wakati wa Mkutano wa Kampeni ya CCM kumnadi Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Mwinyi  uliofanyika katika uwanja wa Mpira Gando Wilaya ya Wete Pemba
WASANII kutoka  Kambini Kichokocho  kijiji cha Mchangamdogo wakicheza ngoma ya msewe wakati wa hafla ya mkutano wa kampeni ya CCM iliofanyika katika uwanja wa mpira Gando Wilaya ya Wete Pemba.
MANJU wa Mkota Ngoma Othman Ali Haji akitowa burudani wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Hussein Mwinyi, uliofanyika katika uwanja wa mpira Gando Wilaya ya Wete Pemba.
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo Flava Said Kitwana ( Mabawa ) akiwa na msanii wa Taarab Fatma Issa wakitoa burudani wakati wa mkutano wa kampeni  ya Mgombea Urais wa Zanzibar  kwa tiketi ya  CCM Mhe.Dk. Hussein mWinyi, iliofanyika katika uwanja wa mpira Gando Wilaya ya Wete Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...