Na Life Shija Dsj
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni mgombea mwenza wa kiti cha urais kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan amewasihi wakazi Wilaya ya Babati kudumisha amani na utulivu katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaofanyika Oktoba 28.

Samia ameyasema hayo wakati akiendelea na kampeni kuelekea Uchaguzi mkuu huko Bashnet Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

“Ili maendeleo yapatikane ni lazima kuendelea utawala bora kudumisha utawala bora ni kujenga amani na kuendeleza amani katika nchi yetu."Amesema Samia.

Hata hivyo amewasisitiza wakazi wa Babati kupiga kura za ndio kwa wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi wakianzia kwa Rais Dkt.John Joseph Magufuli, Madiwani Pamoja na Wabunge wa Chama cha Mapinduzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...