Picha ya pamoja.

Na Samwel Mtuwa - Geita.
KATIBU Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Riziki Shemdoe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome pamoja na Naibu Katibu Mkuu wizara ya Viwanda na Biashara Ndugu Rudovick Nduhiye kwa pamoja wametembelea Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) lililopo katika viwanja vya maonesho ya madini yanayoendelea mkoani Geita.

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Madini walifika katika Banda hilo na kupata maelezo ya kina juu maendeleo ya Utafiti wa Rasilimali Madini unaofanywa na GST 

Kwa umoja wao wamefurahishwa sana na hatua mbalimbali zinazofanywa na GST juu ya utunzaji wa takwimu za madini nchini kwa lengo la kuendeleza sekta ya madini.

Sambamba na hilo , wamefurahishwa pia na hatua iliyopo ya Utafiti wa madini katika maeneo mbalimbali yanayoashiria uwepo wa madini nchini.

Wakizungumza juu ya wazawa kufanya tafiti za rasilimali madini , wamepongeza na kuendelea kuamini kuwa watanzania wenyewe wanaweza kufanya tafiti za jiosayansi ambazo zitaleta tija katika sekta ya uchumi nchini.

Kwa upande Dkt.Mussa Budeba Mtendaji Mkuu wa GST aliwashukuru Makatibu Wakuu hao juu ya kuiamini GST katika tafiti zake za Jiosayansi inazofanya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...