MGOMBEA Ubunge jimbo la madaba mkoani Ruvuma kupitia Chama cha NCCR- Mageuzi bwana Mkinga Ugin Gideon akizungumza mara baada ya kujitoa kinyang'anyiro cha Ubunge katika jimbo alilokuwa akiwania ubunge.
Na Amiri Kilagalila, Njombe
MGOMBEA Ubunge jimbo la madaba mkoani Ruvuma kupitia Chama cha NCCR- Mageuzi bwana Mkinga Ugin Gideon amejitoa katika nafasi ya kushiriki mchakato wa kuwania nafasi hiyo,kwa madai ya kuridhishwa na mwenendo wa uchapa kazi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo chini ya serikali ya awamu ya tano.

Hayo yamebainishwa na mgombea huyo wakati akizungumza na vyombo vya habari mkoani Njombe akiwa ameambatana na mwenyekiti wake wa chama hicho jimbo la madaba mkoani Ruvuma bwana Joseph Kibena ambaye amejiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa Jimbo.

“Nimeamua kujitoa rasmi katika kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha Ubunge jimbo la Madaba mkoa wa Ruvuma kwasababu zifuatazo moja,ni Udhaifu wa mfumo wa vyama vya upinzani kwasababu havina taswira ya kuchukua Dola”alisema Mkinga Ugin Gidion aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Madaba kupitia NCCR-MAGEUZI

Mkinga alitaja sababu ya pili kuwa “ni unafiki wa vyama vya Upinzani tulikuwa tukipiga kelele juu ya miundombinu lakini awamu hii ya tano kila kitu kimefanyika ila bado wapinzania wanaendelea kupinga wakati walikuwa chanzo cha haya yote”alisema Mkinga Ugin Gidion aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Madaba kupitia NCCR-MAGEUZI

Vile vile Mkinga alisema sababu ya tatu “ ni kuridhishwa na uongozi wa Dkt,John Pombe Magufuli,kama CCM watajiskia niamie kwao nipo tayari wakati wowote na nitamuunga mkono Mbunge wangu ambaye yupo kwa kipindi hiki” alisema Mkinga Ugin Gidion aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Madaba kupitia NCCR-MAGEUZI

Aidha mgombea huyo ameeleza hatua za kisheria ambazo mgombea huyo amezichukua katika kujiondoa kwake ikiwemo kupitia kiapo cha mahakama

Joseph Kibena ni mwenyekiti wa chama cha NCCR-MAGEUZI jimbo la Madaba ameunga mkono kauli ya aliyekuwa mgombea wake nafasi ya Ubunge kujiondoa licha kuteuliwa na tume ya taifa ya uchaguzi kushiriki mchakato wa kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao.

“Tumejipima sisi,wale waliogombea na kujilinganisha na wengine na tumeona wale waliopo wanatosha kwasababu tumeona kwa miaka mitano yale waliyotekeleza” alisema Joseph Kibena Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-MAGEUZI Jimbo la Madaba aliyejiuzulu nafasi yake

Aidha ameomba kujiunga na chama cha Mapinduzi“Kwasababu tumejiondoa kwenye Chama cha NCCR-MAGEUZI,tunaomba kama Chama cha Mapinduzi kitaona tunawafaa basi kwa wakati utakaowafaa wao wanaweza kutupokea na kwa mantiki hiyo tumebisha hodi CCM” Joseph Kibena Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-MAGEUZI Jimbo la Madaba aliyejiuzulu nafasi yake

Katika hatua nyingine kituo hiki kimeongea na msimamizi mkuu wa tume ya uchaguzi Jimbo la madaba bwana Fakii Mpenda kwa njia ya simu kwa lengo la kujua ukweli wa jambo hilo ambaye amekiri kupokea barua ya mgombea huyo kujiondoa.

“Alileta barua lakini pia alileta na kiapo kutoka kwa Hakimu kwamba amejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho,na katiba pia inamruhusu kwa utashi wake kujitoa”alisema Fakii Mpenda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...