………………………………………………………… 

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Merdad Kalemani amezindua Mradi wa Ujazilizi Fungu la Pili unaolenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vitongoji ambavyo havina umeme katika vijiji vilivyofikiwa na miundombinu. 

Akizindua Mradi huo katika kitongoji cha Ufuluma Wilaya ya Uyui na Migombani Wilaya ya Nzega Septemba 24, 2020 Dkt. Kalemani alisema vitongoji ambavyo havina umeme vitaanza kusambaziwa umeme sasa. “Mpango halisi wa kuanza kupeleka umeme kwenye vitongoji unaanza rasmi leo hapa katika kitongoji cha Ufuluma mkoani Tabora” alisema. 

Alisema jumla ya vitongoji 1,103 na wateja wa awali 69,079 wataunganishiwa umeme kwa kipindi cha miezi ya tisa ya utekelezaji wa Mradi huo. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Philemon Sengati alitoa wito kwa wananchi kutumia vizuri fursa ya upatikanaji wa huduma ya umeme ili kufanikisha malengo ya Serikali kufikia uchumi wa kati na wa viwanda. 

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo aliwahimiza wananchi kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya kuongeza kipato kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ili kubadili mfumo duni wa maisha ya vijijini. 

Mradi huu unafadhiliwa na Serikli za Tanzania, Norway na Sweden pamoja na Umoja wa Ulaya kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini (REF) na utagharimu Shilingi Bilioni 142. Utatekelezwa katika mikoa tisa (9) ya Dodoma, Kilimanjaro, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Singida, Pwani, Tanga na Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...