Na Jane Edward Arusha,Michuzi TV


Mwanamke Mtanzania mfanyabiashara aishiye Marekani(UK) ,Gladness Katega Amewataka wanawake na wanaume kujitokeza katika kongamano la wajasiliamali linalotarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 2 hadi 6 ili kujifunza na kujadili changamoto za kibiashara ili kuweza kupanua biashara zao na kumuinua mwanamke kiuchumi.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Katega alisema kongamano hilo litawasaidia  wanawake wa Tanzania katika kuinuka kiuchumi na kuweza kutanua biashara zao ikiwa lengo lao Ni kuona wanawake wakifanya biashara kwa pamoja kupitia ushirikiano wa umoja wao.


"Tunataka mwanamke kuinuka  kiuchumi kwa ndani na nje ya nchi  kwani wanawake wajasiriamali wakijitokeza wote na kufanikiwa  kupata elimu Kupitia mafunzo watajadiliana namna ya namna ya kukuza biashara kufikia  biashara nakufikia Mataifa mengine,"alisema Mkurugenzi huyo.


Katika kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira ambapo litadhaminiwa na wadau mbalimbali wakiwemo sunbright hotel,partner Africa Investment,na Kipina beauty saloon ikiwa Hadi Sasa wamejisajili wanawake kutoka nchi mbalimbali zaidi ya 90.


"Kila mwanamke na mwanaume audhurie ili kuwa na mitandao ya kibiashara nakujua namna ya upatikanaji wa masoko pamoja na kutatua changamoto ya namna ya kukuza na upatikanaji wa mitandao kwani ugonjwa wa covid umesitisha shughuli nyingi za kibiashara lakini Kupitia kongamano hilo litawasaidia kupata elimu zaidi,"alisema.


Kwa upande mwezeshaji wa mfunzo ya wanaume ya Kings master class kutoka nchini Kenya ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya RB,Robert Burale alisema wanaume wengi wanatunza  maumivu moyoni na kushindwa kuyasemea kwa watu kuhusu hali ya maisha kitu ambacho hupelekea wanaume kupoteza maisha kwa msongo mawazao.


"Kupitia mafunzo haya wanaume watazungumza maumivu yao yote na kuweza kupeana njia za kutatua ili kumfanya afurahie hali aliyonayo na kuweza kutatua matatizo na maumivu atunzayo moyoni  na kuweza kufanya shughuri zake zote,"alisema Burale.


Katika kongamano hilo watajifunza  pamoja nakutembelea maeneo ya hifadhi katika mbuga za wanyama na kubadilishana mawazo mbalimabali .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...