Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo, Ushirikiano na Sanaa wa ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Cecile Frobert(kushoto)akizungumza  jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kuzungumzia tamasha la wikiendi Live lililoandaliwa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Ufaransa na Nafasi Art Space.Kulia ni Mratibu wa Sanaa za Jukwaani Kwame Mchauru.




Wanamuziki wa kundi la Bahati Band wakitoa vionjo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mkutano wao. Hiyo ni moja ya Band itakayotoa burudani wakati wa tamasha hilo.



Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WASANII zaidi ya 15 wanatarajiwa kushiriki katika tamasha kubwa la muziki wa asili na maonyesho ya sanaa litakalofanyika Jumamosi hii  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa tamasha hilo ambaye pia ni Meneja wa sanaa za maonyesho wa taasisi ya Nafasi Art Space  Kwame Mchauru, amesema tamasha hilo limeandaliwa na taasisi yao kupitia udhamini wa  Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania.

 Amefafanua kwamba kuwa wasanii watakaoshiriki kwenye muziki ni wale wanaopiga muziki wao katika mtindo wa kiasili wakichanganya na vionjo vya kisasa.

Pia kutakuwa na maonyesho mengine ya vitu vya sanaa na kwamba wasanii wengi wa vitu vya asili watakuwepo na wanatarajia ratiba itaanza asubuhi hapo  hapo Nafasi Art Space.

Amewataja  baadhi ya wasanii ambao watakuwepo kutoa burudani kuwa ni Shabo Makota, Bahati Band, Wahapahapa, One the Incredible, Tara Jaza pamoja na Leo Mkanyia.

Aidha, alisema kuwa tamasha hilo limegawanywa katika sehemu mbili ambapo kutakuwa na maonyesho ya sanaa pamoja na sanaa ya jukwaani.

Akizungunza kuhusu tamasha hilo, Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo, Ushirikiano na Sanaa wa ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Cecile Frobert, amefafanua Ubalozi wa ufaransa unaona umuhimu wa kukuza tamaduni na sanaa na ndio sababu ya kushirikiana na Nafasi Art Space kuandaa tamasha hilo.

Amesisitiza ubalozi wa Ufaransa umekuwa ukishrikiana na wasanii mbalimbali na katika kipindi cha mlipuko wa Covid 19 walikuwa wakiendesha programu mbalimbali kwa njia ya mtandao."Tunayo furaha kukutana pamoja kupitia tamasha hili la Jumamosi, tutaendelea kushirikiana kwa karibu na wasanii ili kuendeleza sanaa."

Hata hivyo imeelezwa kuwa tamasha hilo limepewa jina la 'Wikiendi pamoja tena' .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...