Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR) Profesa Yunus Mgaya (aliyesimama)akizungumza katika mkutano wa wadau wa siku mbili wa Utafiti wa HOPE mwishoni mwa wiki hii wilaya Bagamoyo Mkoa wa Pwani ,Walioketi wakimsikiliza ni Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti Dakta.Paul Kazyoba (wa kwanza kushoto)na Mkurugenzi wa Ufatiliaji na Tathimini wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dakta Jerome Kamwela (wa Pili kutoka kushoto)

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha NIMR Mbeya Dakta Nyanda Elias Ntinginya akiwakaribisha washiriki wa mkutano wa wadau wa Utafiti wa Hope wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani,Aliyeketi kushoto kwake ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa NIMR Dakta Ndekya Oriyo - NIMR Mbeya imebobea katika tafiti za Ukimwi na Kifua Kikuu na Magonjwa mengine ya kuambukiza.

Mratibu wa utafiti kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI (NACP), Dokta. Werner Maokola akichangia hoja katika mkutano wa wadau wa HOPE (Hope Study) uliomalizika mwishoni mwa wiki Bagamoyo mkoani Pwani.
Wadau katika mkutano wa siku mbili Utafiti wa Hope uliofanyika mwishoni mwa wiki hii wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Wadau wa Utafiti wa Hope (HOPE Study) kutoka NIMR ,TACAIDS na NACP katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha mjadala wa matokeo ya awali ya Utafiti huo .Matokeo kamili ya Utafiti wa HOPE yanatarajiwa kukamilishw mwezi Desemba 2020 ambapo yatatolewa rasmi.

Na Chalila Kibuda, Bagamoyo Pwani
MKURUGENZI Mkuu wa NIMR Prof. Yunus Mgaya amempongeza Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha NIMR Mbeya Dakta Nyanda Elias Ntinginya kwa umahiri wake katika kusimamia na kuratibu utekelezaji wa miradi ya utafiti ukiwemo utafiti wa HOPE unaolenga katika kuimarisha shughuli za upimaji wa Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa Watoto wachanga waliozaliwa na akina mama wenye maambukizi ya VVU; hatua ambayo imekiwezesha kituo hicho cha NIMR Mbeya kufikia malengo ya miradi yake kwa wakati na utimilifu.

Profesa Mgaya amesema taarifa ya matokeo ya awali ya utafiti wa HOPE inaashiria kuwa mradi huo utachangia kuimarisha udhibiti wa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au wakati wa kunyonyesha.

Akizungumza mjini Bagamoyo mkoani Pwani katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa HOPE uliolenga kujadili matokeo ya awali ya utafiti wa mradi huo; Profesa Mgaya amesema ushirikishwaji mzuri wa wafanyakazi katika mradi na matumizi sahihi na ya wakati ya fedha; yamechochea kwa kasi utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajiwa kutoa matokeo yake rasmi ifikapo mwezi Desemba 2020.

“NIMR Mbeya iko mstari wa mbele kutumia ubunifu katika utekelezaji kazi za kitafiti na kujengea uwezo watafiti na viongozi wake wakiwemo viongozi wa miradi hatua ambayo inaashiria kuleta matokeo chanya ya kisekta na Taifa kwa ujumla hata katika mradi huu wa HOPE.” Alifafanua Profesa Mgaya.

Utafiti wa HOPE unafanywa na NIMR kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) chini ya ufadhili wa Global Fund na ulianza kutekelezwa rasmi mwezi April 2020. Utafiti huu unatekelezwa katika mikoa 18 ya Tanzania bara ndani ya wilaya 44.

Katika hatua nyingine Profesa Mgaya ameiomba Serikali kuendelea kutenga fedha zaidi za utafiti katika maeneo ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria ili kuwezesha nchi kuendeleza kikamilifu tafiti zake hata baada ya wafadhili kumaliza muda wao.

Amewataka wataalam wa maabara nchini kujituma na kujifunza matumizi mapana zaidi ya mashine za GeneXpert zilizopo katika hospitali mbalimbali ili kuhakikisha kuwa zinatumika pia katika kupima Virusi Vya Ukimwi kwa watanzania wakiwemo watoto na siyo Kifua kikuu tu kama ilivyotambulika hapo awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...