Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kigoma 

RAIS wa Burundi Evarist Ndayishimiye amesema kuwa ana uhakika Dk.John Magufuli ambaye kwa sasa yupo kwenye kampeni atashinda katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu. 

Akizungumza leo katika Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma baada ya kupokelewa kwa mizinga 21 kama kuonesha heshima kwake ikiwa ni mara yake ya kwanza kuja nchini tangu kuteuliwa kuwa Rais wa nchi hiyo, Rais Ndayishimiye amesema ana uhakika katika uchaguzi unaokwenda kufanyika Oktoba 28 mwaka huu Dk.Magufuli atashinda kwa kura nyingi. 

Amesema Rais Magufuli ameibadilisha Tanzania na Kigoma imebadilika."Nakupongeza sana kwani Kigoma mimi sio mgeni ila imebadilika sana, imejengeka.Najua uko kwenye kampeni na nina uhakika utashinda uchaguzi tena sana, na Warundi wanasema wangekuwepo hapa wangemchagua Dk.Magufuli.Wewe na Watanzania ni kama baba na watoto, hivyo nina uhakika utashinda. 

Wakati huo huo akifafanua kuhusu ujio wake, amesema sio kwamba amekuja kama rafiki bali amekuja Tanzania kwasababu wao wanaamini watanzania ni wazazi wao tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na alikuwa akienda bega kwa bega na muasisi wa taifa lao la Burundi. 

Ameongeza wakati wa machafuko ya Burundi, nchi ya Tanzania ilikubali kubeba msalaba wa Burundi kwa kuwapokea wakimbizi, na wale waliokaa muda mrefu walipewa uraia hivyo ametoa shukrani kwa Rais Magufuli na Watanzania wote. 

"Mimi unavyoniona hapa , nakuona wewe kama baba yangu, nimekuja kusoma kwako nijue nafanya nini.Tanzania wanaijua sana Burundi, Tanzania imetuonea huruma ikasema itusogeze kidogo Bandari ya Dar es Salaam, na Burundi tuko tayari kufanya kazi kwa bidii. 

"Hatutarudi nyuma tena kwenye machafuko ya zamani,na najua Burundi tukiwa na amani, Kigoma watafurahi sana kwani hawatakuwa wakipata usumbufu. 

Awali Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi amesema leo ni siku maalum kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Burundi kutokana na ujio wa ziara ya kikazi wa Rais Evarist Ndayshimye nchini. 

“Rais Ndayshime tangu achaguliwe hii ndio ndio nchi yake kuja, hivyo kwa Tanzania hiyo ni heshima kubwa sana na tunakushukuru Rais Ndayshimye kwa kuja nchini,”amesema Waziri Kabudi.

Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye akizungumza na Wananchi katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...