MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua,kutembelea miradi ya maji kujionea namna unavyotekelezwa eneo la Horohoro Mkinga mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa maelekezo ya Rais Dkt John Magufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribu zaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani na mazingira ya miundombinu pamoja na kuzindua mtambo wa umeme jua uliosimikwa hapo kwa ajili ya kusukuma maji wilayani Mkinga kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari.
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la World Vision,Damian Sanka kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela kushoto wakati alipotembelea
mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Duga Maforoni wenye thamani ya Sh milioni 471 uliojengwa na shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Japan.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akiwa tayari kuzindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Duga Maforoni wenye thamani ya Sh milioni 471 uliojengwa na shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Japan.
Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la World Vision,Damian Sanka kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela kushoto wakati alipotembelea
mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Duga Maforoni wenye thamani ya Sh milioni 471 uliojengwa na shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Japan.


MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akimtiwsha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Duga Maforoni Mwanasha Salim mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Duga Mtandikeni


Bwawa ambalo ndio chanzo cha maji katika mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Duga Maforoni.
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella amelishukuru Shirika la World Vision Tanzania kwa kushiriakiana na Serikali ya Japan kuwekeza katika mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Duga Maforoni wenye thamani ya Sh milioni 471.

Amesema kuwa hatua hiyo inaunga mkono juhudi za Rais Dk John Magufuli mkoani Tanga katika kuondoa changamoto ya maji ambapo mwaka huu serikali kupitia Wizara ya Maji imetoa kiasi cha Sh Bilioni 11 katika kutekeleza miradi ya maji vijijini mkoani hapa.

Mkuu huyo wa mkoa yupo katika ziara ya wiki moja mkoani Tanga ya kukagua miradi mbalimbali ya maji kuona utekelezaji wake pamoja na kutoa maagizo ambapo ameambatana na Meneja RUWASA mkoa mhandisi Upendo Omari,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Tanga,Mhandisi Geofrey Hilly pamoja na wataalamu wa maji kutoka mamlaka hiyo.

Akiwa katika eneo la mradi huo,Mkuu wa Mkoa alikagua,kutembelea mazingira ya miundombinu hiyo pamoja na kuzindua mtambo wa umeme jua uliosimikwa hapo kwa ajili ya kusukuma maji.

Katika mradi huo, shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Japan limesaidia kujenga miundombinu mipya ya kisasa ya maji safi katika chanzo cha maji katika bwawa ikiwemo kutenga eneo maalum la kunyweshea mifugo,ujenzi wa matenki ya kuhifadhia maji pamoja na kufunga mtambo mkubwa wa umeme jua ambao utakuwa unasaidia kusukuma maji pindi umeme unapokatika.

Ametoa wito kwa wananchi wa kijiji hicho kuyatumia maji hayo vizuri pamoja na kulinda na kutunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

“Wafugaji na wananchi kwa ujumla natoa rai kuilinda miundombinu hii na kuyatumia haya maji vizuri ili yatusaidie wote kwa muda mrefu,”alisema.

Mwenyekiti wa kijiji hicho,Ally Mohamedi Kizanda amesema kuwa shirika hilo kupitia ujenzi wa mradi huo wameondokana na changamoto kubwa ya maji haswa umeme ulipokuwa unakatika kutokana kabla ya hapo hawakuwa na matenki ya kuhifadhia maji,mtambo ulikuwa unasukuma moja kwa moja kwenye mabomba na umeme ulipokuwa unakatika maji yalikuwa hayapatikani na pia gharama kubwa za ankara ya umeme.

“Tunawashukuru World Vision kwa mradi huu,kabla ya hapo hatukuwa na matenki wala mtambo wa umeme jua changamoto ilikuwa kubwa,sasa hivi tunapata maji safi kwa muda wa saa 24 yanatoka katika vituo vyote 25 kijijini,”alisema.

Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la World Vision,Damian Sanka amesema kuwa hadi kukamilika kwa mradi huo takribani wananchi 3,339 wa kijiji cha Maforoni wananufaika na mradi huo.

Amesema kuwa kabla ya ujenzi wa mradi huo,watoto haswa wanafunzi walikuwa na changamoto ya ufaulu wa masomo shuleni kutokana sehemu kubwa walikuwa wanawasaidia wazazi wao katika kutafuta maji,hivyo kukamilika kwa mradi huo kutaondoa changamoto hiyo kutokana uwepo wa mtambo wa umeme jua umefanikisha maji kupatikana muda wote kijijini hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...